Katibu wa klabu ya waandishi
wa habari (Singpress) mkoa wa Singida Bw. Abby Nkungu akitoa taarifa
yake ya utekelezaji kwa kipindi cha mwaka uliopita.
Mkutano
Mkuu wa mwaka wa Klabu ya Waandishi wa habari (Singpress) Mkoani
Singida, umeagiza uongozi wa zamani wa Klabu hiyo, kukabidhi ofisi
katika kipindi cha wiki mbili, vinginevyo uchukuliwe hatua kali zikiwemo
za kisheria.
Mkutano
huo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Wilaya ya
Manyoni mjini, Umeagiza uongozi huo uandikiwe barua rasmi ya kuupa muda
wa wiki mbili kuanzia
tarehe ya barua husika.
Akitoa
pendekezo hilo mbele ya mkutano huo mkuu, Shabanj Msangi, amesema
pamoja na muungano wa jumuiya ya vilabu vya waandishi wa habari nchini
(UTPC), kuridhia uongozi wa sasa kuingia ofisini bila makabidhiano,
uamuzi huo ni kinyumbe na katiba ya Singpress.
Baada
ya mvutano mkali kwa upande uliokuwa unapendekeza juu ya hatua ya
kukabidhi rasmi ofisi na upande uliokuwa ukidai kwamba hatua hiyo haina
mashiko au tija, zilipingwa kura na upande uliokuwa unataka uongozi wa
zamani uliokuwa chini ya uenyekiti wa mchungaji Emmanuel Barnaba
ukabidhi ofisi, ulishinda.
Katika
hatua nyingine, mkutano huo katika hali isiyokuwa ya kawaida, uliamua
kusamehe deni la shilingi milioni 2,217, 600 ambalo walikuwa wanadaiwa
wanachama waliokodisha vifaa vya klabu ikiwemo kamera.
Baadhi
ya wanachama walidai kwamba kutokana na udhaifu mkubwa ulionyeshwa na
uongozi uliopita, basi madeni hayo ambayo yameacha vifaa
vilivyokodishwa kuharibika na kupelekea visitumike tena, basi madeni
yafutwe na wasidaiwe wanachama hao.
Wanachama
hao waliokodisha vifaa hivyo,walikodishwa vikiwa vipya havijatumika
kabisa na vimekaa mikononi mwao hadi vikaharibika na havitegenezeki
tena.
Baada
ya mvutano huo mkali kudumu zaidi ya nusu saa, upande uliopendekeza
madeni hayo yafutwe na yasionekane kwenye kumbukumbu za Klabu,
ulishinda.
Mapendekezo
hayo yawaligawa wananchama wa Singpress katika vipande viwili na baadhi
walidai kuwa kitendo cha kusamehe madeni hayo ni sawa na kuifanya
Singpress kuwa ni shamba la bibi.
Uamuzi
huo uliendelea kulaumiwa kwa madai kwamba msamaha wa aina hiyo usiokuwa
na tija, utakuwa endelevu kwa vile wakopaji au watumiaji wa mali ya
Klabu watakuwa wanautumia katika kuihujumu Klabu kiuchumi.
Wadaiwa
hao na madeni yao kwenye mabano ni Doris Mehgji, (90,000/=), Elisante
Mkumbo (25,000/=), Jumbe Ismail (1,431,600), Hillary Shoo (615,000) na
Evarist Thomas (56,000).
Hata hivyo Hillary Shoo kwa sasa sio mwanachama wa Singpress.
No comments:
Post a Comment