Kamanda wa polisi mkoa wa
Singida, Linus Sinzumwa akionyesha silaha za jadi zilizokuwa zinatumiwa
na majambazi yaliyoteka gari la SUA no.SU 37012 na kuporwa zaidi ya
shilingi 19.8 miloni na mali mbali mbali nje kidogo ya mji wa Singida.
Jeshi
la polisi mkoani Sngida limefanikiwa kuwakamata watu 25 wanaotuhumiwa
kuteka gari la Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) mjini Morogoro na kisha
kupora watu waliokuwa wanasindikiza maiti kupeleka mkoani Mara kwa ajili
ya mazishi.
Gari lililotekwa ni Land Cruiser SU 37012 lililokuwa likiendeshwa na Kalistus Mapulila.
Katika
utekaji huo, inadawa kuwa jeneza lililokuwa limebeba mwili wa marehemu
Munchari Lyoba mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo cha SUA,
lilifumuliwa na mwili wa marehemu ukasachiwa.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa, amesema kwa sasa majina ya
watuhumiwa hao hayawezi kutangazwa hadharani kwa madai kuwa kitendo
hicho kinaweza kuathiri shughuli za upelelezi ambao bado unaendelea.
Amesema watuhumiwa wengi ni wakazi wa kijiji cha Kisaki kilichopo katika manispaa ya Singida.
Kamanda
huyo amesema katika msako huo mkali ambao bado unaendelea, mbali na
kukamatwa kwa watuhumiwa hao, pia baadhi ya mali iliyoporwa ikiwemo nguo
za waathirika, kamera, laptop na simu, zimekamatwa.
Ametaja
vitu vingine vilivyokamatwa ni pamoja na vitambulisho vya kazi, charger
mbili za simu, kadi aina ya tembo kadi na shilingi 20,500 zizookotwa
eneo la tukio.
Amesema
mafanikio hayo makubwa yamechangiwa na ushirikiano mkubwa kutoka kwa
wananchi ambao ulipelekea kazi ya kukamata watuhumiwa,kuwa rahisi na
nyepesi.
Kamanda
Sinzumwa ameongeza kuwa baadhi ya watuhumiwa baada ya kugawana shilingi
milioni 19.8 walizopora, walianza kunywa pombe ovyo huku wakijitapa
kuwa wana uwezo mzuri wa kiuchumi.
Kamanda
ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ambao
utasaidia mkoa wa Singida kuendelea kuwa eneo lenye utulivu na amani
wakati wote.
Aidha,
ameitaka TANROADS mkoa wa Singida kufanya juhudi za makusudi kuondoa
mawe mengi makubwa yalioko kandokando ya barabara ambayo majambazi
wanayatumia katika azma yao ya kuteka magari.
Wakati
huo huo, Kamanda huyo amewahakikishia wakazi wa mkoa wa Singida, kuwa
kipindi chote cha kuelekea siku kuu za Xmas na mwaka mpya, kutakuwa na
amani na utulivu wa hali ya juu.
No comments:
Post a Comment