Tuesday, December 18, 2012

SAJUKI AANGUKA JUKWAANI ARUSHA

 Sajuki akitafakari kwa kina mara baada ya kuanguka chini ya jukwaa huku wenzake wakimpa pole
 msanii wa filamu nchini,Sajuki akiwa ameshikwa na wasanii wenzake mara baada ya kuanguka jukwaani juzi ndani ya uwanja wa Sheikh Amri katika tamasha la wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wale wa filamu.
msanii wa filamu nchini,Sajuki akiwa ameshikiliwa na wenzake wakimshusha chini ya jukwaa mara baada ya kuanguka alipopewa nafasi ya kuwasalimia mashabiki wake


HALI ya msanii  wa filamu nchini,Juma Said Kilowoko maarufu kama Sajuki imeelezwa si ya kuridhisha  mara baada ya msanii huyo juzi kuanguka jukwaani mara baada ya kuishiwa nguvu wakati alipopewa

Kesi ya Vigogo wa CHADEMA wanaodaiwa kumtukana Mbunge wa Iramba yaendelea kupigwa danadana yaahirishwa hadi leo.

 Vigogo wa CHADEMA Dkt. Kitila Mkumbo mshauri wa CHADEMA na mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar-es-salaam (kulia) katibu wa sera na utafiti wa CHADEMA makao makuu Mwita Waitara (katikati) na Pela Ngunangwa aliyejitambulisha kuwa ni dereva kiongozi ofisi za CHADEMA makao makuu, wakiwa wanaelekea kuingia kwenye mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida.
Wakili wa vigogo wa CHADEMA Raymond Kimu (wa kwanza kushoto aliyenyoosha kidole) akiteta na wateja wake Mwita Waitara (katikati) na wa pili kulia mwenye miwani Dk.Kitila Mkumbo.

 Kesi inayowakabili vigogo wa CHADEMA ya kumtolea lugha ya matusi mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi  (CCM) Mwigulu Lameck Nchemba, iliyoanza kusikilizwa jana kwenye mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida imeahirishwa hadi leo.  
Kesi hiyo imeahirishwa baada ya kukosekana kwa hati za

Waandishi 17 mkoani Singida wapatiwa mafunzo ya biashara na uchumi na kutakiwa kujiendeleza kielimu.

 Mkufunzi Mnaku Ambani akitoa mafunzo ya biashara na uchumi yaliyohudhuriwa na waandishi wa habari 17 wa mkoa wa Singida. Mafunzo hayo ya siku nne yalifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa katoliki mjini Singida.
Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Singida wakimsikiliza kwa makini mkufunzi Mnaku Ambani (hayupo kwenye picha) akitoa mada zake za biashara na uchumi.

 Wanachama wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Singida(Singpress), wamehimizwa kufanya juhudi za makusudi kumiliki ardhi ili pamoja na mambo mengine, kujijengea mazingira mazuri ya

Monday, December 17, 2012

Serikali Wilayani Singida yazindua awamu ya pili ya kampeni ya Vita dhidi ya Jangwa.

 Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi akizindua upandaji miti katika kijiji cha Kitope manispaa ya Singida.

 Mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi akishiriki kampeni ya kupanda miti ili kuokoa wilaya hiyo isikumbwe na balaa la Jangwa.


 Mtoto Juma Sungi wa darasa la tatu katika shule ya msingi ya Mwankoko manispaa ya Singida akishiriki kampeni ya kupanda miti kwa lengo la kunusuru manispaa hiyo isigeuke jangwa.
Mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi akionyesha miche ya miti maji ambayo amedai kuwa inatumika kuvuna mbao na pia kutengenezea sabuni.

 Serikali wilayani Singida imepiga marufuku mara moja uvunaji ovyo wa misitu, kwa madai kwamba uvunaji wa aina hiyo, unatishia

Sunday, December 16, 2012

TFDA yakamata bidhaa zilizomaliza muda wake Mkoani Singida.

 Maafisa TFDA kanda ya kati, Florent Kyombo (kushoto) akishuhudia mmiliki wa duka la Temba, Singida mjini Bw. Temba akisaini fomu yakutekeza bidhaa zilizoisha muda wake na akazitoa dukani, TFDA walimsifu sana.
Kaimu meneja TFDA kanda kati, Florent Kyombo na Joseph Mwasambili wakikagua vinywaji vikali kwenye moja ya duka mjini Singida, katika oparesheni maalumu kusaka bidhaa zilizomaliza muda kwa matumizi ya binadamu.

 Mamlaka ya chakula na dawa nchini (TFDA), imekamata bidhaa mbalimbali ikiwemo vipodozi vilivyopigwa marufuku na vilivyomaliza muda vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh. Milioni

Dkt. Kone awataka wakuu wa wilaya Singida kuhakikisha watoto wanapata chanjo mbili mpya za Rotavirus na PCV 13.

 Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone akizungumza kwenye mkutano maalum wa uhabarishaji juu ya umuhimu wa chanjo mpya za Rotavirus inayokinga maradhi ya kuharisha na PCV 13,inayokinga ugonjwa wa Nimonia.Chanjo hizo ambazo ni mpya,zinatarajiwa kuanza kutolewa kuanzia Januari mwakani.
Mkuu wa wilaya ya Iramba.Yahaya Nawanda akichingia mada juu ya chanjo mpya za totavirus na PCV 13 kwenye mkutano maalum kwa lengo la kuhabarisha juu ya chanjo hizo.

 Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone amewaagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wanawahamasisha wananchi juu ya umuhimu wa watoto wao kupata chanjo mbili mpya, za Rotavirus na PCV 13 ili kujikinga na magonjwa  ya

Wednesday, December 12, 2012

Watu 25 mbaroni mkoani Singida kufuatia tukio la kupora fedha na kisha kuvunja jeneza na kusachi maiti.

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, Linus Sinzumwa akionyesha silaha za jadi zilizokuwa zinatumiwa na majambazi yaliyoteka gari la SUA no.SU 37012 na kuporwa zaidi ya shilingi 19.8 miloni na mali mbali mbali nje kidogo ya mji wa Singida.


Jeshi la polisi mkoani Sngida limefanikiwa kuwakamata watu 25 wanaotuhumiwa kuteka gari la Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) mjini Morogoro na kisha kupora watu waliokuwa wanasindikiza maiti kupeleka mkoani Mara kwa ajili ya mazishi.
Gari lililotekwa ni Land Cruiser SU 37012 lililokuwa likiendeshwa na Kalistus Mapulila.
Katika utekaji huo, inadawa kuwa jeneza lililokuwa limebeba mwili wa marehemu

Tuesday, December 11, 2012

Wahandishi wa habari mkoa wa Singida wagawanyika, mkutano mkuu wautaka uongozi wa zamani kukabidhi ofisi ndani ya wiki mbili.

Katibu wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida Bw. Abby Nkungu akitoa taarifa yake ya utekelezaji kwa kipindi cha mwaka uliopita.


Mkutano Mkuu wa mwaka wa Klabu ya Waandishi wa habari (Singpress) Mkoani Singida, umeagiza uongozi wa zamani wa Klabu hiyo, kukabidhi ofisi katika kipindi cha wiki mbili, vinginevyo uchukuliwe hatua kali zikiwemo za kisheria.
Mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Wilaya ya Manyoni mjini, Umeagiza uongozi huo uandikiwe barua rasmi ya kuupa muda wa wiki mbili kuanzia

Sunday, December 9, 2012

MAITI YASACHIWA NA KUPORWA ZAIDI YA MILIONI 19 NA MAJAMBAZI


 Gari aina ya Land Cruiser mali ya chuo cha SUA cha mjini Morogoro kama linavyoonekana baada ya kupigwa mawe na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi nje kidogo ya mji wa Singida.
Mhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida ambaye jina lake halikuweza kutambuliwa mara moja, akiliweka sawa jeneza baada ya kufanyiwa ukarabati baada ya kubomolewa na majambazi na kulisachi.


Watu wasiofahamika idadi yao na ambao wanadhaniwa kuwa ni majambazi, wamevamia gari lililokuwa linasafirisha maiti kutoka Morogoro mjini hadi mkoa wa Mara na kupora  zaidi ya shilingi milioni 19.8.
Baada ya kumaliza zoezi la uporaji huo, majambazi hayo yalishusha jeneza na kisha...

Saturday, December 8, 2012

Kampuni ya Tan Discovery yakanusha kutowasaidia wachimbaji wadogo wa madini mkoani Singida.

Afisa msimamizi wa kampuni ya Tan Discovery Akida Sungura akiwa Internet Cafe akitekeleza majukumu yake.


Kampuni ya Tan Discovery inayojishughulisha na kuuza na kukodisha vifaa vya uchimbaji madini kwa wachimbaji wadogo mkoani Singida, imekanusha taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba haijawasaidia wachimbaji kufikia

Madhehebu ya dini jimbo la Singida yamtwisha mgana msindai mzigo wa kutokomeza rushwa ndani ya CCM.

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Izumbe Msindai akizungumza kwenye mkutano wa viongozi wa madhehebu ya dini jimbo la Singida mjini.Kushoto ni mwenyekiti wa CCM jimbo la Singida mjini Hamisi Nguli na wa pili kulia ni katibu wa CCM mkoa wa Singida,Naomi Kapambala.
 Mmoja wa viongozi wa madhahebu ya dini,mzee Omari Hamza akitoa kero alizokuwa nazo kwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai (hayupo kwenye picha).
Baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini waliohudhuria mkutano ulioitishwa kwa ajili ya mwenyekiti wa CCM mkoa kujitambulisha kwao na wao kutoa kero ushauri ya maoni kwa lengo la kuendeleza manispaa ya Singida.


Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini jimbo la Singida mjini wamemwomba Mwenyekiti mpya wa CCM  mkoa wa Singida Mgana Izumbe Msindai, kuweka mikakati madhubuti itakayokomesha vitendo vyote vya rushwa ili

Tuesday, December 4, 2012

Diwani kata ya Ikungi Singida (CHADEMA) amesema ripoti ya uwajibikaji haitochakachuliwa kamwe.

 Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida Manju Msambya (aliyesimama) akitangaza kuahirishwa kwa mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaji katika halmashauri ya wilaya ya Singida.Wa tatu kutoka kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida na wa pili kushoto ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida Alli Nkhangaa.
 Pichani juu na chini ni Baadhi wa wadau wa maendeleo wa halmashauri ya wilaya ya Singida wakimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya ya Ikungi,Manju Msambya (hayupo pichani) wakati akiahirisha mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaji.

 Mmoja wa maafisa kutoka shirika lisilo la kiserikali la Sikika akikusanya ripoti zilizosababisha kuahirishwa kwa mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaji katika halmashauri ya wilaya ya Singida.
Kiongozi wa timu ya shirika lisilo la kiserikali la Sikika Mahindi Simon akieleza kusikitishwa kwake kuahirishwa kwa mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaji.


Diwani wa viti maalum (CHADEMA) tarafa ya Ikungi wilayani Ikungi mkoani Singida Tedi Daghau, amesema pamoja na halmashauri ya wilaya ya Singida kusogeza mbele mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaki, haitakuwa na ubavu wa  ‘kuichakachua’ ripoti hiyo kwa lengo la.....

Jamii yaombwa kusaidia makundi maalumu yasiyojiweza.

 Mkuu wilaya Iramba-Singida, Yahaya Nawanda akikabidhi msaada wa madaftari kwa mwanafunzi Hilda Samwel (12) uliotole na vikundi vitatu vya jumuiya ya kuweka na kukopeshana (SELC).
DC Iramba Yahaya Nawanda akimkabidhi mwanafunzi Jacob David (11) wa shule msingi Kiomboi hospitali msaada wa madaftari uliotole na vikundi vitatu vya jumuiya ya kuweka na kukopeshana (SELC).


Mkuu wa wilaya Iramba mkoani Singida, Yahaya Nawanda ameitaka jamii kusaidia makundi yasiyojiweza, wakiwemo watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, ili kujenga moyo wa upendo baina yao.
Nawanda alisema hayo wakati akikabidhi vifaa mbalimbali vya shule msingi, kwa ajili ya wanafunzi wa shule sita  za watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi, wilayani humo.
Msaada huo ulitolewa na.....

Monday, December 3, 2012

.Kamati ya Siasa ya CCM mkoa wa Singida yachagua wajumbe wake na kutoa ujumbe kwa wataalam wa kilimo kuhakikisha pembejeo zinawafikiwa wakulima kwa wakati.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai akitoa taarifa yake ya uchaguzi wa kamati ya siasa ya mkoa kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha)


Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida kimechagua kamati yake ya siasa mkoa katika uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai, amewataja wajumbe wa kamati hiyo, kuwa ni

Wilaya ya Iramba Mkoani Singida yangoza kwa maambukizi ya VVU kwa kipindi cha Januari hadi Septemba 2012.

 Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Singida Edson Mdala akitoa taarifa yake kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika kimkoa Singida mjini.
 Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida na DC wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi akihutubia wananchi waliohudhuria maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika kwenye kituo cha zamani cha mabasi mjini Singida.
 Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida,Queen Mlozi (wa kwanza kulia) akiwa amewasha mshumaa kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika kimkoa Singida mjini.Wa pili kulia ni meya wa manispaa ya Singida Sheikh Salum Mahami.
 Mratibu wa shirika la PSI mkoa wa Singida Daniel Mainoya (mwenye maiki) akitoa maelezo juu ya shughuli zinazofanywa na PSI kwa kaimu mkuu wa mkoa wa Singida Queen Mlozi (wa kwanza kulia).
 Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida Queen Mlozi (kulia mwenye suti) akikagua banda la Takukuru wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani zilizofanyika kimkoa Singida mjini.
 Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida Queen Mlozi (mwenye suti) akishiriki kutoa burudani na watu wanaoishi na virusi (VVU) wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika kimkoa katika manispaa ya Singida.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika kimkoa manispaa ya Singida.


Wilaya ya Iramba mkoa wa Singida inaongoza kwa maambukizi mapya ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa UKIMWI kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu.
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone, wakati akizungumza kwenye

Sunday, December 2, 2012

SHARO MILLIONEA ASABABISHA BONGE LA BIFU KATI YA DJ CHOKA NA LADY NAAA AKA MTOTO MLITO.





 Haya ni maneno ambayo lady naaa aka mtoto mlito alimwandikia Dj Choka kwenye BBM

Hichi ndicho DJ CHOKA aliandika kwenye account ya ke ya facebook kumjibu lady naah "UJUMBE HUU UKUFIKIE WEE UNAYEJIITA LADY NAH...Nilikaa kimya na nikakuvumiliaaaaa baada ya kupata ujumbe wako mfupi ulioutuma BBM, ukaona haitoshi jana ukaenda...

Saturday, December 1, 2012

MAITI YA SHARO MILLIONEA ALIKATWA VIDOLE NA VIBAKA...

Watu wa nne wamekamatwa na jeshi la police wakiwa na Baadhi ya vitu alivyokuwa navyo marehemu Sharo Milionea kama vile

TAZAMA JINSI SHARO MILLIONEA ALIVYOPATA AJALI.

 Gari alilokua akiendesha Sharo Millionea lilianza kutoka nje ya barabara hapa
 Sehemu gari lilipokwenda kusimama ni pale kwenye watu wengi panaonekana kwa mbali.



 Gari lilivuka hii sehemu na kubinukia kule mbele baada ya hilo daraja dogo ambako ndio liligonga huu mti hapa chini.
 Huu ni mti ambao aliugonga katikati akaukata kuwa vipisi viwili, mwingine ukatupwa mbele ya huu kama unavyoonekana alafu gari ikaenda kubinuka kichwa chini miguu juu kwenye lile eneo la wazi unaloliona kwa mbali baada ya hayo matawi ya huo mti hapo mbele.
                                            kipisi cha pili cha mti aliouvunja katikati.

 Hapa ndipo gari lilikuja kusimama na Sharo Milionea akiwa peke yake kwenye gari alirushwa nje.
Hapa ndipo mwili wa Marehemu ulikutwa baada ya kutupwa kutoka kwenye gari, mashuhuda waliofika kwenye eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali wanasema walianza kuwatafuta majeruhi wakidhani ni wengi na hawakumuona mtu yeyote kwenye gari