Wednesday, September 25, 2013

Halmashauri za Wilaya na Manispaa waaswa kutotoza ushuru kwa ‘Lumbesa’

 Mkuu wa wilaya ya Singida, mwalimu Queen Mlozi akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada  mizani za vipimoaina mbalimbali  iliyotolewa na wakala wa vipimo uliopo chini ya wiraza ya viwanda na biashara kwa lengo la kupiga vita magunia maarufu kwa jina la Lumbesa.Wa pili kulia ni kamishina msaidizi wa wakala wa vipimo,Peter Samwel Masinga na wa kwanza kulia ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida, Elia Digha.
 Kamishina msaidizi wa wakala wa vipimo,Peter Samwel Masingida akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa mizani ya aina mbalimbali iliyotolewa msaada na wakala wa vipimo kwa ajili ya kukabiliana na tatizo sugu la gunia maarufu kwa jina la Lumbesa.Wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Singida,mwalimu Queen Mlozi na kulia ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida na diwani wa kata ya Msange, Elia Didha.
 Kamishina msaidizi wa wakala wa vipimo Peter Samwel  Masinga (kulia)akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Singida,mwalimu Queen Mlozi moja ya mizani iliyotolewa na wakala wa vipimo kwa ajili ya kukabiliana na gunia aina ya lumbesa linalodaiwa kuwadhulumu wakulima jasho lao.
 Mkuu wa wilaya ya Singida,mwalimu Queen Mlozi (kushoto) akimkabidhi mstahiki meya wa manispaa ya Singida moja ya mzani uliotolewa na wakala wa vipimo kwa lengo la kutokomeza gunia maarufu kwa jina la lumbesa linalodaiwa kuwapunja mapato wakulima.
Mkuu wa wilaya ya Singida, mwalimu Queen Mlozi (kushoto) akimkabidhi makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Singida na diwani wa kata ya Msange,Elia Digha moja ya mzani uliotolewa msaada na wakala wa vipimo kwa lengo la kutokomeza gunia aina ya Lumbesa.

Halmashauri za Wilaya na Manispaa Mkoa wa Singida, zimeaswa kutotoza ushuru kwa kutumia kipimo cha ‘gunia’ ambacho kimedaiwa kushawishi wafanyabiashara na wasafirishaji kutumia kitendo hicho cha kujaza gunia maarufu kama ‘Lumbesa’ kwa lengo la kulipa ushuru kidogo.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Kamishina Msaidizi wa Wakala wa Vipimo Ndugu Peter Samwel Masinga,wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi mizani za viwango mbalimbali ambazo zimetolewa  kwa msaada na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Msaada huo umetolewa kwa halmashauri ya wilaya na manispaa ya  Singida Ndugu Masinga  amesema matumizi ya kipimo cha kutumia gunia kutoza ushuru yalibainika juni mwaka huu wakati afisa mtendaji mkuu wa wakala wa vipimo, Magdalena Chuwa alipotembelea mkoa wa Singida.

Masinga alisema halmashauri kuendelea kutoza ushuru kwa kutumia kipimo cha
gunia badala ya mizani, kitendo hicho kinasababisha vita ya kutokomeza matumizi ya Lumbeza, kuwa ngumu kupindukia.

“Halmashauri na manispaa zinapaswa kuacha mara moja matumizi ya kutumia gunia na badala yake watumie vipimo stahiki ili wananchi pamoja na wakulima waweze kunufaika na kazi yao ya kilimo.

Pia wafanyabiashara na wasafirishaji nao wahimizwe kutumia vipimo na waache kabisa kutumia gunia kama kipimo”,alifafanua.

Katika hatua nyingine, Masinga aliwataka wakulima kuanzisha umoja, ili kuwa na nguvu zaidi itakayowawezesha kuwakataa wafanyabiashara kuendelea kuwapangia na kuwaandalia bei na pia kuwalazimisha matumizi ya Lumbesa.

“Napendekeza elimu itolewe kwa wakulima juu ya umuhimu wa kuwa na umoja wao, ili pamoja na faida nyingi za umoja huo, watumie nguvu ya umoja  huo, kuuza mazao yao ndani na nje ya nchi iliwaweze kufaidika zaidi na shughuli zao za kilimo”,amesema Masinga.

Aidha, amesema kuwa wakala wa vipimo, utaendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa matumizi sahihi ya vipimo.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mwalimu Qeen Mlozi amesema zinahitajika nguvu za pamoja katika kuhamasisha wakulima ili fedha wanazopata kutokana na uuzaji wa mazao yao,zinatumika vizuri kwa lengo la kuinua hali zao za kiuchumi.


Aidha aliwataka  wakulima kuwakataa  wafanyabiashara wa ndani na nje ya mkoa,wenye tabia ya kununua  mazao wakiwa bado yapo shambani.

No comments:

Post a Comment