Friday, September 20, 2013

Serikali ya Mkoani Tabora imewaagiza madiwani kusimamia kikamilifu fedha za umma

 Katibu tawala mkoa wa Tabora, Kudra Mwinyijuma akizungumza kwenye hafla ya kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga Protace Magayane Kwa sasa Magayane ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida. Pia katika hafla hiyo iliyofanyika Igunga mjini,mkurugenzi mpya wa halmashauri ya Igunga, mwalimu Rustika Turuka alikaribishwa rasmi.Wa kwanza kulia (walioketi) ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi,Protace Mgayane na anayefuatia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, Abubakari Shaban.
 Katibu tawala mkoa wa Tabora, Kudra Mwinyijuma (kulia) akimkabidhi mweka hazina wa halmashauri ya wilaya ya Igunga,Gordon Julius Dinga,cheti maalum baada kuiwezesha halmashauri hiyo kupata hati safa ya mahesabu kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2010/2011 na 2011/2012.
 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Abubakari Shaban akitoa nasaha zake kwenye halfla iliyofana ya kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, Protace Magayane aliyehamia wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida. Pia kumkaribisha mkurugenzi mpya wa halmashauri ya Igunga, mwalimu Rustika Taruka.Wa pili kushoto ni mkurugenzi Protace Magayane na wa kwanza kushoto ni mke wake mkurugenzi Magayane.
 Aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga,Protace Magayane akitoa nasaha zake wakati akizungumza kwenye hafla ya yeye kuagwa na viongozi na wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga.
 Mkurugenzi wa halmashauri mpya ya Ikungi mkoa wa Singida, Protace Magayane (kushoto) akijadiliana mambo ya Afisa wake wa Kilimo Ayubu Sengo wakati wa hafla ya kuagwa (Magayane) iliyofanyika Igunga mjini.
 Baadhi ya viongozi na wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoa wa Tabora, wakipata msosi kwenye hafla ya kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, Protace Magayane na kumkaribisha mkurugenzi mpya wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, mwalimu Rustika Turuka.Hafla hiyo ilifanyika  Igunga mjini.
Mtaalam wa kufungua champeni wa wilaya ya Igunga ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja akifungua Shampeni  kwenye hafla ya kumuaga aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, Protace Magayane na kumkaribisha mkurugenzi mpya mwalimu Rustika Turuka.

SERIKALI mkoa wa Tabora,imewaagiza madiwani wa Halmashauri ya Wilaya na Manispaa,kusimamia kikamilifu matumizi ya mali za umma ikiwemo fedha, kwa kuzingatia kanuni,taratibu na sheria za nchi.

 Hatua hiyo itasaidia pamoja na mambo mengine,Halmashauri kupata hati safi za mahesabu ya fedha za umma.

 Changamoto hiyo imetolewa juzi na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora,Kudra Mwinyimvua,wakati akizungumza kwenye sherehe ya kupongezana watumishi wa Halmashauri ya Igunga kwa kupata hati safi kwa miaka miwili mfululizo (2010/2011 na 2011/2012).

 Alisema dawa pekee ya kuwa na uhakika wa halmashauri kupata hati safi,ni kuimarisha usimamizi wa ndani wa matumizi ya mali za umma ikiwemo fedha za umma.

 Mwinyimvua alisema usimamizi huo pia utasaidia utoaji huduma bora zitakazokidhi matarajio ya wananchi na utekelezaji  wa miradi mbalimbali ya wananchi kuwa ubora unaofanana na fedha za umma zilizotumika.

 “Kwa halmashauri ya Igunga,nitumie jioni hii kuwapongeza kwa dhati kabisa madiwani na watendaji kwa juhudi zao zilizofanikisha halmashauri kupata
hati safi kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo”,alisema katibu tawala huyo na kuongeza;

 “Pongezi pekee zimwendee Mkurugenzi Protace Magayane (kwa sasa amehamishiwa halmashauri ya Ikungi mkoa wa Singida) kwa juhudi zake binafsi za kuwaunganisha madiwani na watendaji kufanya kazi za umma kama mnyororo kitendo kilichosaidia kuiletea halmashauri maendeleo endelevu”.

 Aidha,Mwinyimvua alitumia fursa hiyo kumtakia kila la kheri mkurugenzi Magayane katika kuwatumikia wananchi wa wilaya mpya ya Ikungi mkoani Singida.


Sherehe hiyo iliyofana ilitumika pia kumuaga mkurugenzi Magayane aliyehamia wilaya ya Ikungi na kumkaribisha mkurugenzi mpya mwalimu Rustika Turuka

No comments:

Post a Comment