Monday, November 18, 2013

Bima ya Afya yaanda kongamano kwa wadau wake Singida.

Meneja mfuko wa Taifa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Singida, Agnes Chaki (wa kwanza kushoto) akitoa taarifa kwa mwandishi wa habari wa MOblog (hayupo kwenye picha) juu ya kufanyika kwa kongamano la wadau 250 wa Mfuko wa Taifa Bima ya afya (NHIF) Mfuko wa Afya ya jamii (CHF)linalotarajiwa kufanyika kesho (13/11/2013) kwenye ukumbi wa mikutano wa hotel ya Katala Beach mjini Singida.Wa kwanza kulia ni mhasibu wa NHIF,Godlessen Bellium (mhasibu) na katikati ni Isaya Shekifu (Afisa matekelezo na uratibu NHIF mkoa wa Singida.
Jengo la ofisi ya Mfuko wa Taifa Bima ya Afya (NHIF) mkoani Singida.

MFUKO wa Taifa Bima ya Afya (NHIF) kwa ushirikiano na mfuko wa afya ya jamii (CHF) mkoani Singida,unatarajia kufanya kongamano kubwa la wadau wake kesho (leo 13/11/2013) asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano wa hotel ya kitalii ya Katala Beach (KBH) iliyopo mjini hapa.

Akizungumza na MO blog ofisini kwake leo,meneja wa NHIF mkoa wa Singida,Agnes Chaki,alisema kongamano hilo litakalofunguliwa na mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Vicent Kone, litaanza mapema saa mbili asubuhi.

Alisema kuwa kongamano hilo la aina yake la kwanza kufanyika mkoani hapa, linatarajiwa kuhudhuriwa na wadau 250.

Chaki alitaja baadhi ya wadau hao kuwa ni pamoja na katibu tawala mkoa,wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa halmashauri na manispaa,wabunge wote,waheshimiwa madiwani na waganga wakuu wa wilaya.

“Wengine ni wakuu wa vyombo vya usalama,viongozi wa dini,waratibu wa bima za afya wa halmashauri (NHIF na CHF,wawakilishi wa  wanachama wa mfuko,waajiri walioandikishwa na mfuko,watoa huduma na waandishi wa habari”,alisema meneja Chaki.

Alisema kuwa dhumuni la kongamano hilo,ni kutoa fursa kwa wadau wa
mifuko hiyo kubadilishana uzoefu na pia kujadiliana masuala muhimu yahusuyo bima ya afya na changamoto mbalimbali zinazoikabili mifuko hii ili kupata ufumbuzi utakaoimarisha utendaji wa mifuko hii,inayohudumia Watanzania walio wengi.

No comments:

Post a Comment