Tuesday, November 5, 2013

Halmashauri ya Ikungi Singida yakusanya Tsh 154.9m ndani ya miezi mitatu.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi,Protace Magayane akifafanua jambo mbele ya kikao cha kawaida cha madiwani.Katikati ni mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Seelestin Yunde na wa kwanza kulia ni mwenyekiti CCM wilaya ya Ikungi, Hassan Tati.
Baadhi ya watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi,wakifuatilia kwa makini ajenga zilizokuwa zikizungumzwa kwenye kikao cha kawaida cha baraza la Madini.
Diwani wa viti maalum Perpetua Nkuwi,akichangia ajenda iliyowasilishwa kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi.
Mbunge (CHADEMA) wa jimbo la Singida mashariki,Tundu Lissu akichangia ajenda zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi.
Mbunge (CCM) wa jimbo la Singida magharibi, Mohammed Missanga akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya Ikungi.

Halmashauri  ya Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida imekusanya mapato ya zaidi ya shilingi 154.9m kutoka vyanzo vyake mbalimbali vya mapato kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Septemba mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mweka Hazina wa Halmashauri hiyo Celestine Muttashobya wakati akitoa taarifa yake mbele ya kikao cha madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika mjini Singida.

Amesema makusanyo hayo ni sawa na asilimia moja ya lengo la kukusanya mapato ya zaidi ya shilingi 16.9 bilioni kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2013/2014.

Akifafanua, Muttashobya amesema kati ya fedha hizo mapato ya ndani ya halmashauri yenyewe wamekusanya shilingi 57,757,484/m

“Serikali kuu imetupa ruzuku ya shilingi 30 milioni kufidia kodi na ushuru uliofutwa Pia serikali kuu imetupatia ruzuku ya zaidi ya shilingi 53 milioni kwa ajili ya matumizi yasiyo ya mishahara na zingine zaidi ya shilingi 14.1m  kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi”,amesema.

Mweka Hazina huyo amesema katika kipindi hicho cha miezi mitatu wametumia shilingi 59,853,962.26m sawa na asilimia tatu ya lengo la kutumia shilingi 16,106,933,419/m.

Katika hatua nyingine Muttashobya alitaja kata tatu za jimbo la Singida mashariki zilizofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na asilimia iliyokusanywa kwenye mabano kuwa ni
Siuyu (25),Mng’onyi (19) na Mkiwa (19).

Alitaja kata tano zilizofanya vibaya katika ukusanyaji wa mapato na asilimia ya makusanyo kwenye mabano kuwa ni Kikio (0), Unyahati (1), Lighwa (2), Misughaa (3) na Ikungi (7).

Kwa upande wa jimbo la Singida magharibi Mweka Hazina huyo alitaja kata tatu zilizofanya vizuri katika kukusanya mapato kuwa ni Iyumbu (88),Minyughe (61) na Mugungira (43).


Muttashobya alitaja kata tano zilizofanya vibaya kuwa ni Iseke (0), Irisya (5), Muhintiri (8), Ighombwe (10) na Kituntu (12).aaaaaaaaaaa

No comments:

Post a Comment