Wednesday, November 20, 2013

Chuo Cha Utumishi wa Umma kuongeza matawi zaidi.

Mtendaji mkuu wa chuo cha utumishi wa umma Tanzania, Said Nassor kitoa taarifa yake kwenye mahafali ya 16 ya chuo hicho yaliyofanyika mjini Singida. Jumla ya wahitimu 1,909 kutoka chuo cha Tabora na Singida walihitimu katika ngazi mbalimbali.
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone akitoa nasaha zake kwenye mahafali ya 16 ya chuo cha utumishi wa umma Tanzania yaliyofanyika mjini Singida.Kulia aliyekaa,ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma Tanzania, Mh.Celina Kombani ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Tanzania,Celina Kombani akizungumza kwenye mahafali ya 16 ya chuo cha Utumishi wa Umma Tannzania mjini Singida.
Baadhi ya wahitimu wa chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania,waliohitimu mafunzo yao.

WAHITIMU wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania wameagizwa kutumia elimu walioipata kufanya kazi kwa ufanisi ili kuleta tija kwa lengo la kukuza na kuendeleza uchumi wa nchi.

 Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Tanzania, Celina Kombani, wakati akizungumza kwenye sherehe ya mahafali ya 16 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, mjini hapa.

 Aliwaasa kuwa wawe watendaji wazuri mara watakapoanza kazi,na hiyo iende sambamba na kuzingatia kanuni , sheria na taratibu za utumishi wa umma.

 “Tekelezeni majukumu yenu kwa ufanisi kwa kuonyesha uwezo wa kumudu majukumu,uadilifu  na kutoa huduma bora kwa wananchi na sio kufanya kazi kwa mazoea, ili kukamilisha lengo la serikali la kupata matokeo makubwa sasa” amesema Kombani

 Awali Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Said Nassor, amesema wana mkakati wa kupanua vyuo vyake ambapo mwakani wanaanzisha tawi jipya mkoani mbeya.

 Aidha, amesema pia mwakani wanatarajia kuongeza madasa katika tawi la tabora na wataanza ujenzi wa Tawi la chuo cha mkoa wa singida.

 “kwa ujenzi wa tawi la mkoa wa singida, tayari tumekamilisha zoezi la la kulipa fidia kiasi cha shilingi
260 milioni kwa wakazi ambao awali walikuwa wamiliki wa eneo husika. Pia tunatarajia kuanza maandalizi ya michoro ya kutuo kikuu cha chuo cha Ikwiriri” amesema

  Kuhusu uboreshaji wa huduma, ali sema chuo kinaendelea na uboreshaji wa huduma za maktaba na maabara za kompyuta, ununuzi wa magari manne pamoja na kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wa chuo.


 Kwa mujibu wa Nassor, jumla ya wahitimu 1,909 kutoka chuo cha Singida na Tabora, wamehitimu kozi ya cheti cha uhazili  msasa , ngazi ya cheti cha awali, ngazi ya cheti na ngazi ya dpiploma.

No comments:

Post a Comment