Tuesday, November 19, 2013

Mbaroni kwa kuvujisha mtihani wa kidato cha nne.

           Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida, ACP Geofrey Kamwela.

JESHI la polisi mkoa wa Singida, linawashikilia walimu wawili kwa tuhuma ya kuvunjisha matihani wa kidato cha nne unaoendelea kufanyika hivi sasa nchini kote.

Walimu hao ni walimu wa shule ya sekondari kata ya Nkinto wilaya ya Mkalama mkoani Singida, ambao ni mwalimu mkuu wa shule hiyo Monica Sebastian (30) na mwalimu Agaloslo Otieno (32).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida, ACP Geofrey Kamwela, amesema kuwa tukio hilo limetokea novemba 13 mwaka huu kati ya saa tatu na tatu usiku katika shule ya sekondari ya Nkinto kata ya Mwangeza tarafa ya Kirumi wilaya ya Mkalama.

Amesema kuwa mwalimu Agaloslo akiwa anasimamia mtihani katika shule ya sekondari ya Mwangeza, alikuwa anaandika baadhi ya maswali ya masomo ya Kiswahili na Civics  kwenye simu yake ya kingajani na kumtumia mwalimu wake mkuu Monica akiwa shuleni kwake Nkinto.

Kamwela alisema baada ya Monica kupata maswali hayo,alikuwa anayatafutia majibu akiwa chooni na wanafunzi walikuwa wanamfuata huko huko chooni kupewa majibu hayo.

“Lengo lao ilikuwa ni kuwasaidia wanafunzi ili waweze kufanya vizuri katika mtihani wao wa kidato cha nne mwaka huu.Wanafunzi wenywe waliisha ambiwa kuwa wawe wanadanganya kwamba wanaenda kujisadia chooni,ili wakapatiwe majibu na mwalimu mkuu”,alifafanua kamanda na kuongeza;

“Uchunguzi wa awali wa polisi unaonyesha kuwa uvunjishaji huo ulifanyika kwa nyakati tofauti kati ya mwalimu mkuu Monica na mwalimu wake Agaloslo akiwa ana simamia mtihani huo katika shule nyingi.Baada ya mwali mkuu kutumiwa maswali alikuwa anajificha ndani ya choo cha shule yake na watahiniwa kwa nyakati tofauti huomba ruhusa kwa wasimamizi kwenda chooni kwa nia ya kujisaidia na hapo humkuta mwalimu mkuu huyo na kuwapa maelekezo ya namna ya kujibu maswali hayo”.

Amesema baada ya Polisi kupata taarifa ya siri kutoka kwa wasamaria wema, waliweka mtego katika shule ya sekondari ya Nkinto na kufanikiwa kumkamata mwalimu
Monica huku simu yake ikiwa na baadhi ya maswali ya mtihani.


Alisema kwa sasa bado wanaendelea na upelelezi zaidi na mara utakapomalizika,watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayowakabili.

No comments:

Post a Comment