Friday, November 22, 2013

WAHAMASISHWA KUTUMIA VYOO BORA ILI KUZUIA MAGONJWA YA MILIPUKO.



BAADHI YA VYOO BORA MKOANI SINGIDA.
Kata ya Mtamaa Manispaa ya Singida inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa vyoo bora hali inayoweza kusababisha kutokea kwa magonjwa ya miripuko ikiwemo kipindupindu.

Uchunguzi uliofanywa na Singida Yetu Blog katani hapo umebaini kuwa kati ya kaya tano hadi kumi ni kaya moja tu ndiyo yenye choo bora huku kaya nyingine zikiwa zinatumia vyoo visivyo bora na nyingine kutumia vyoo vya majirani au vya taasisi za elimu kama vile shule.

Baadhi ya wakazi walihojiwa na standard radio wamesema kukosekana kwa vyoo bora kumesababishwa na kukosekana kwa elimu huku wengine wakisema vyoo vingi vilibomolewa na mvua zilizonyesha mwanzoni mwa mwaka huu

Akizungumzia tatizo hilo Diwani wa kata hiyo Bw. Gwae Mbua amesema kuwa kwa kuanza wameanza kuweka msisitizo katika shule kuwa na vyoo bora na baada ya kukamilika mpango huo utahamia katika
makazi ya wananchi ambapo sheria zimewekwa kwa wale watakao kiuka maagizo ya kuwa na vyoo bora. 

No comments:

Post a Comment