Thursday, November 14, 2013

Wanachama 51 wa Chadema wahamia CCM kata ya Mungaa, Singida.

Wanakikundi cha uhamasishaji cha kata ya Mungaa jimbo la Singida mashariki, wakitoa burudani kwenye hafla ya uzinduzi wa shina la wakereketwa wa CCM la Mzambarauni katika kijiji cha Makiungu.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu  CCM (NEC) taifa wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Jonathani Njau ameivunja ngome ya CHADEMA kata ya Mungaa, baada ya wanachama wake 51 kukihama na kurejea CCM.

 Wanachama hao ambao karibu wote ni vijana, katika risala yao wamedai wamehama CHADEMA, baada ya kubaini kuwa wanatumiwa vibaya na wanasiasa wa chama hicho.

 Wamedai kwamba wanasiasa wa CHADEMA wamejaa uchu wa madaraka, wanatumia uongo mkubwa, hila, kupandikiza chuki na wanatoa ahadi  za uongo katika kupata uongozi.

 “Kabla na baada ya uchaguzi, tuliahidiwa ahadi nyingi na viongozi wa CHADEMA kumbe ahadi zote hizo ni ahadi hewa.Vijana tumekwisha kuwagundua na hatudanganyiki tena.Kwa sababu sisi ni nguvu kazi ya taifa,tunatakiwa kutumika kwa maslahi ya taifa na si kwa maslahi ya mtu binafsi”,inasema sehemu ya risala yao.

 Katika hatua nyingine,vijana hao walishangiliwa kwa nguvu na umati uliohudhuria mkutano huo wa hadahara,wakati wakiimba wimbo maalum ambao ulidai kwamba CHADEMA ni sawa na kitanda cha kamba kilichojaa kunguni na hivyo,hakilaliki.

 Akizungumza muda mfupi baada ya kuzindua shina la wakereketwa  la Mzambarauni  waliorejea CCM, Mnec  Njau amesema mlango wa CCM upo
wazi wakati wote kupokea wanaCCM waliokimbilia upinzania na kurejea CCM  chama pekee ambacho sera zake zinatelekezeka.

 Amesema hivi sasa kuna wimbi kubwa la wanaCCM waliokimbilia upinzani wanarejea nyumbani CCM,baada ya kubaini kwenye upinzania na hasa CHADEMA, kumejaa chuki, uwongo uliopitliza na wananchi wanakatazwa kuchangia maendeleo yao.

 Aidha, Njau ambaye kitaaluma ni mwanasheria, amewahimiza wakazi wa jimbo la Singida mashariki kuwapuuza watu/viongozi wanaowadanganya wasichangie maendeleo yao.

 “Kama tutaendelea kuwaamini wapotoshaji hawa,wilaya ya Ikungi itakuwa tanuru la kuzalisha  vijana/watu bumbumbu hasa kwenye masomo ya sayansi, kwa sababu  hatutaki kuchangia ujenzi wa maabara katika shule zetu za sekondari za kata”, alifafanua MNEC huyo.


 “Katika karne hii ya sayansi na teknolojia, mtu mwenye akili timamu hawawezi kugoma kuchangia ujenzi wa vyumba vya maabara,ili mtoto wake aweze kupata fursa nzuri ya kujisomea masomo ya sayansi kwa ufanisi mkubwa”, amesema Njau.

1 comment:

  1. YETU MACHO.KAMA UBUNGE UNAPATIKANA KWA KUWATUKANA WENZENU BASI J.NJAU UMEPATA MZEE.ILA WATU WA MAKIUNGU SI WAJINGA WANAUTAMBUA MCHEZO.WALISHACHANGA SANA ILA VIONGOZI WAKAJINEEMESHA.HAKIKA IKUNGI AMA WATU WA SINGIDA SI WAGUMU KUCHANGIA MAENDELEO YAO LAKINI MBMA PESA ZINALIWA NA EXECUTIVE HAIWASAIDII!NIRA YA CCM HAWATAJITWIKA TENA LABDA KUSIWE KABISA NA WAGOMBEA WA UPINZANI.NA WALE VIJANA NI WA RIKA LANGU NA WENGINE NI WADOGO NAWAJUA VZR SI KWEL NI WANACHADEMA BALI WALE NI POLITICAL ROBOTS.AMINI MANENO YANGU.MWAMBIE J.NJAU YEYE HANA TATIZO ILA JOHO ALILOVAA NA KAMA ANATAKA UBUNGE AKAMWOMBE M.MISANGA AMWACHIE HAPA BADO MAJI MAREFU.

    ReplyDelete