Wednesday, February 26, 2014

Halmashauri ya Singida yatumia shilingi 89 milioni kugharamia ujenzi wa soko.

Naibu waziri Fedha na Uchumi na Mbunge wa jimbo la Iramba magharibi, Lameck Nchemba Mwigullu, akizindua jengo la soko la kisasa la kijiji cha Old Kiomboi wilaya ya Iramba.

HALMASHAURI ya wilaya ya Iramba mkoani Singida imetumia zaidi ya shilingi 89 milioni kugharamia ujenzi wa soko la kisasa la kijiji cha Old Kiomboi.

Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji wa kijiji cha Old Kiomboi,Betha Nakomolwa wakati akitoa taarifa yake kwa Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi na Mbunge wa jimbo la Iramba magharibi,Lameck Nchema Mwigulu aliyezindua soko hilo.

Amesema katika fedha hizo,nguvu kazi ya wanaqnchi,imeokoa zsaidi ya shilingi 8.9 milioni.

Aidha,Nakomolwa amesema Mwigulu amechangia shilingi 7,200,600,mchango wa kijiji (CDG) shilingi 28,550,000,Tasaf awamu ya kwanza hadi ya nne,shilingi 44,379,700 na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida,shilingi laki nne.

Katika hatua nyingine,Afisa Mtendaji huyo,amesema ujenzi wa matundu matatu ya choo cha soko hilo ambao unatarajiwa kugharimu shilingi milioni

Tuesday, February 25, 2014

Mbaroni kwa mauaji ya makusudi ya kitoto kichanga.

 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela.

JESHI la Polisi mkoani Singida linamshikilia Naomi Daud (20) mkazi wa kitongoji cha Mahawa kata ya Mungumaji tarafa ya Unyambwa Manispaa ya Singida kwa tuhuma ya kumuuawa mtoto wake mara baada ya kujifungua.

Imedaiwa Naomi baada ya kujifungua,alimnywesha mtoto wake maji ya mvua lita moja na kusababisha kifo chake papo hapo.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida,SP.Cordula Lyimo amesema tukio hilo la kusikitisha limetokea februari nne mwaka huu usiku wa nane huko katika kata ya Unyambwa Manispaa ya Singida.

Amesema siku ya tukio,Naomi akiwa chumbani kwao na mama yake mzazi,alijifungua bila kusaidiwa na mtu na mama yake alikuwa akiangalia kitendo hicho kama sinema.

“Mara baada ya kumaliza kujifungua,mtuhumiwa aliweza kumnywesha kichanga hicho

DC Singida awataka Madiwani na watendaji wa kata hadi Mei 30 Ujenzi wa Maabara uwe umekamilika.

 Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mwashinga Mlozi, akizungumza na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Singida.Pamoja na mambo mengine, aliagiza kwamba Diwani na mtendaji wake wa kata wasipomaliza ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara kabla ya Mei 30 mwaka huu, atawachukulia hatua kali ya kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani. Wa pili kulia (aliyeketi),ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Singida,Illuminata Mwenda na anayefuata ni mwenyekiti wa halmashauri ya Singida.

MKUU wa wilaya ya Singida,Queen Mwashinga Mlozi,amewatahadharisha madiwani na watendaji kata,kwamba kabla ya mei 30 mwaka huu wawe wamekamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara,vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Mlozi ametoa agizo hilo wakati akizungumza mbele ya kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kilichofanyika mjini Singida.

Alisema madiwani na watendaji kata ambao watashindwa kumaliza ujenzi huo kabla ya muda uliopangwa,watawajibishwa ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani.

“Nitafanya hivyo kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa chini ya kifungu cha 14 na 15 vya sheria za tawala za mikoa na serikali za mitaa ya mwaka 2002 ya kuvunja amri halali ya kutokujenga vyumba vitatu vya maabara”alifafanu mkuu huo wa wilaya.

Dc Mlozi alitaja shule za kata ambazo ujenzi wake

Monday, February 24, 2014

Halmashauri ya Manispaa ya Singida yapongezwa kwa kujenga daraja.

 Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone,(wa kwanza kushoto) akipata maelezo kutoka mkandarasi wa daraja la Mwankoko manispaa ya Singida,Rogers Mchau(anayenyoosha mkono) juu ya maendeleo ya ujenzi wa daraja kijiji cha Mwankoko.

Dk.Kone alilikagua daraja hilo baada ya kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa, kulalamika kwamba fedha zinazotumika katika ujenzi huo ni nyingi hazifanani na daraja lenyewe. Baada ya kulikagua,alikiri kuwa daraja hilo lina thamani na fedha zilizotumika na kwamba bado kuna zaidi ya shilingi 192 milioni zinahitajika ili kukamilisha ujenzi huo.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone,akikagua ujenzi wa daraja la kijiji cha Mwankoko manispaa ya Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akitoa maelekezo juu ya kuboresha ujenzi wa daraja la kijiji cha Mwankoko manispaa ya Singida.
 Daraja la kijiji cha Mwankoko linaloendelea kujengwa na mkandarasi Rogers Mchau.
Mkuu wa mkoa wa Singida (kushoto) akizungumza na Meya Mstahiki wa manispaa ya Singida,Sheikh Salum Mahami wakati alipokuwa akimaliza kukagua ujenzi wa daraja la kijiji cha Mwankoko.
MKUU wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone,ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Singida,kwa juhudi zake za kujenga daraja linalolingana na thamani ya fedha iliyotumika.

 Dk.Kone ametoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki wakati akikagua ujenzi wa daraja hilo, ulioanza rasmi desemba 12 mwaka 2011 na ulitarajiwa kukamilika novemba 14 mwaka 2012.Daraja hilo linaunganisha kata ya Mwankoko na kata ya Mtamaa.

Amesema kuwa fedha ambayo imetumika hadi sasa ya zaidi ya shilingi 216.1 milioni,thamani ya fedha hiyo inafafanana kabisa na kazi ya ujenzi iliyofanyika.

 “Kwa kweli mmefanya kazi nzuri pamoja na mkandarasi wenu.Fedha ambazo mmeziomba serikali kuu ili mmalizie ujenzi wa daraja hili,tutakuwa nyuma yenu katika kuhakikisha mmezipata,ili ujenzi uweze kukamilika kwa mujibu wa mkataba wenu”,amesema.

Mapema Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Joseph Mchina,amesema mradi huo wa ujenzi wa daraja hilo,fedha zake zimetoka katika mfuko wa barabara kupitia OWM-TAMISEMI,zikiwa ni fedha za maombi maalum ya ujenzi wa madaraja.

 Katika hatua nyingine,Mchina amesema hadi sasa ujenzi huo wa daraja,

Mifuko ya Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Singida yahimizwa kuwa makini kwa madai ya kughushi.

Meneja wa NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki, akifungua kikao cha waratibu wa mfuko wa Taifa Bima ya Afya na wale wa mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambacho kilitumika kukumbushana juu ya utoaji huduma bora kwa wananchama.Kulia ni afisa matekelezo na uratibu NHIF mkoa wa Singida,Isaya Shekifu na kushoto ni Edwin Mwangajilo afisa udhibiti ubora NHIF.
Afisa matekelezo na uratibu wa mfuko wa taifa wa Bima ya Afya (NHIF)  mkoa wa Singida, Isaya Shekifu akitoa mada yake kwenye kikao cha wataribu wa mfuko wa NHIF na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) mkoa wa Singida.Kikoa hicho kililenga kubadilishana uzoefu juu ya utendaji kazi,ili kuboresha zaidi huduma za mifuko hiyo.Kushoto ni meneja wa NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki.
Afisa udhibiti ubora NHIF mkoa wa Singida, Edwin Mwangajilo,akitoa mada yake kwenye kikao cha waratibu wa NHIF na CHF kilichofanyika  kwenye ukumbi mdogo wa mikutano wa kanisa katoliki mjini Singida.Kushoto ni meneja NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki.
Baadhi ya waratibu wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na wale wa mfuko wa Afya ya Jamii mkoa wa Singida, waliohudhuria kikao cha kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi, ili kuboresha huduma zaidi.
WARATIBU wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) mkoani Singida,wamehimiza kuwa makini zaidi kukabiliana na wimbi la madai ya kughushi, kwa madai kwamba vitendo hivyo,vitachangia kudhoofisha huduma zinazotolewa na mifuko hiyo.

Wito huo umetolewa na meneja wa NHIF mkoa wa Singida,Agnes Chaki,wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha waratibu wa NHIF na CHF mkoani hapa, kilichofanyika kwenye ukumbi mdogo wa mikutano wa kanisa katoliki mjini hapa.

Alisema kuna baadhi ya watoa huduma si waaminifu  na wanaleta madai ya kugushi, na mfuko umejiandaa kikamilifu kuhakikisha unadhibiti vitendo hivi ili kutimiza lengo la msingi la kuwapa huduma bora wanachama wake

“Ninyi waratibu ninawaomba ndugu zangu, tusaidiane katika kupambana na hili tatizo.Mnapokutana na watoa huduma,naomba mjaribu kuwaelimisha kuwa wawe wanatibu kwa kuzingatia miongozo ya NHIF na ile ya wizara.Wahakikishe kile wanachokitoa kinakuwa ni sawa na wanacho wasilisha NHIF….mfano katika dawa”,alisema Chaki.

Aidha,meneja huyo wa mkoa, alisema mwanachama,mratibu au kiongozi ye yote akisikia au kuona  kuna vitu/vitendo vinafanyika kinyume na taratibu za NHIF,tafadhali atoe taarifa mapema ofisi za NHIF mkoani hapa,ili ziwezekufuatiliwa mapema kabla havijaleta madhara kwa mfuko.

Kwa upande wake afisa matelekezo na uratibu NHIF mkoa wa Singida,Isaya Shekifu,akitoa mada yake ya majukumu ya waratibu wa NHIF/CHF,aliwataka waratibu hao kuhakikisha

Thursday, February 20, 2014

TRA Singida yapandisha Kizimbani Wafanyabiashara.

Jengo la ofisi kuu mamlaka ya mapato (TRA) mkoa wa Singida iliyopo mjini Singida.

MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) Mkoa wa Singida imewapandisha kizimbani wafanyabiashara wanne wa mjini Singida kwa makosa mbalimbali, ikiwemo kutotumia kwa makusudi mashine za kieletroniki (EFD) kukusanyia kodi, huku wakijua wazi ni kosa kisheria.

Shitaka lingine linalowakabili wafanyabiashara hao akiwemo Sabra Mohammed na Khalfani Juma ni kushindwa kulipa kodi ya VAT kwa makusudi, katika vipindi tofauti tofauti kati ya mwezi februari mwaka jana hadi januari mwaka huu, jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya TRA, kifungu namba 148 cha mwaka 2008.

Mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya mkoa Singida Joyce Minde, ilidaiwa na afisa sheria mwandamizi wa TRA kanda ya kaskazini Geva Masele kuwa, wakati washitakiwa wakiendelea na biashara zao katika eneo la barabara ya Karume mjini Singida, walifanya makosa hayo na hivyo kuikosesha serikali mapato.

Hata hivyo washitakiwa wote walikana mashitaka yao na wapo nje kwa dhamana ya Sh. Milioni mbili kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja na shauri hilo litatajwa tena februari 26 mwaka huu.

Wakati huo huo Robert Mkoma anayefanya biashara zake katika barabara ya Lumumba mjini Singida, amefikishwa mbele ya hakimu mkazi wilaya Singida Flora Ndale, kwa shitaka la kushindwa kulipa

Diwani wa CCM kizimbani kwa lugha ya matusi.

Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Singida.

DIWANI wa kata ya Unyambwa (CCM) Halmashauri ya Manispaa ya Singida,Shaban Salum Satu amepandishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Singida akituhumiwa kuwatolea lugha ya matusi maafisa wa Polisi ikiwemo kudai ni ‘mizigo’.

Diwani huyo alifikishwa mahakamani kwa kosa la kutoa lugha ya matusi hivi karibuni anatarajiwa kupandishwa tena kwenye mahakama hiyo kwa tuhuma ya kushiriki kuchoma moto basi la Mtei lililogongwa pikipiki iliyokuwa inatumiwa na watu wanne wa familia moja kwenda shambani.Wanafamilia watatu,walipoteza maisha papo hapo.

Baadhi ya lugha ya matusi inayodaiwa kutolewa na diwani huyo,ni “nyinyi wasege tu,

Mbaroni kwa kukutwa na meno ya Tembo.

                    Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela.

JESHI la Polisi Mkoa wa Singida limefanikiwa kumkamata George James (30) mkazi wa kijiji cha Mwamagembe tarafa ya Itigi wilaya ya Manyoni mkoa wa Singida kwa tuhuma ya kumiliki kinyume cha sheria nyara za serikali vipande 21 vya meno ya tembo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela amesema wamefanikiwa kumkamata George februari 13 mwaka huu saa 2.30 asubuhi huko katika kizuizi cha mazaoa ya misitu na chakula kilichopo katika kijiji cha Ukimbu kata ya Mgandu,tarafa ya Itigi,wilaya ya Manyoni.

Amesema mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia gari aina ya toyota hieze T.797 CQL kusafirisha nyara hizo kutoka kijiji cha Mwamangembe kwenda Itigi mjini.

“Baada ya kufanya upekuzi makini,vijana wangu waliweza kuzikuta nyara hizo zikiwa kwenye

Sunday, February 16, 2014

Viongozi wa umma wahimizwa kushirikiana na wasimamizi wa utafiti.

Baadhi ya wadadisi na wasimamizi wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi 2014 wakisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa kwenye mafunzo yao yaliyomalizika mjini Singida.Wadadisi na wasimamizi hao wametoka mkoa wa Kigoma,Tabora,Singida na Dodoma.
Katibu tawala mkoa wa Singida,Lina Hassan (wa pili kulia walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadadisi na wasimamizi wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi mwaka 2014.Kushoto ni Afisa takwimu mkoa wa Singida Mazinza na anayefuata ni mwakilishi wa mkurugenzi mkuu,ofisi ya taifa ya takwimu Bakilla Bakilla na kulia ni mwakilishi wizara ya kazi na ajira,Thomas Saguda.

VIONGOZI wote wa serikali na wa ngazi zote katika mikoa ya Kigoma,Singida,Tabora na Dodoma,wamehimizwa kutoa ushirikiano,kuhamasisha na kuelimisha umma, umuhimu wa kushirikiana na wadadisi na wasimamizi wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2014.

Imedaiwa kuwa hatua hiyo itasaidia kufikiwa kwa urahisi kwa lengo la serikali ambalo ni kujua soko la ajira nchini lilivyo hivi sasa.

Wito huo umetolewa juzi na Katibu Tawala mkoa wa Singida,Liana Hassan wakati akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo ya siku 14 ya wadadisi na wasimamizi wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi mwaka 2014.Wadadisi na wasimamizi hao,wametoka mikoa ya Kigoma,Tabora,Singida na Dodoma.

Amesema umma wakijua umuhimu wa utafiti huo,watakuwa tayari kutoa

Jeshi la Polisi lahimizwa kuendesha kwa ufanisi madawati ya jinsia ili haki itendeke.

Mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi akisoma hotuba ya Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Jasmine Kairuki kwenye kilele cha maadhimisho ya kupinga ukeketaji duniani yaliyofanyika kitaifa ijiji cha Ngimu wilaya ya Singida.Wa kwanza kushoto,ni mwakilishi wa jumuiya ya kikiristo Tanzania (CCT),Mary Shuma.
Mwakilishii wa jumuiya ya kikiristo Tanzania (CCT), Mary Shuma, akitoa taarifa yake kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji duniani yaliyofanyika kitaifa katika kijiji cha Ngimu wilaya ya Singida.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Ngimu wilaya ya Singida,wakifuatailia matukio yaliyokuwa yakijiri kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kupinga ukeketaji duniani yaliyofanyika kitaifa katika kijiji cha Ngimu.

NAIBU Waziri wa Sheria na Katiba Angellah Jasmine Kairuki amelihimiza Jeshi la Polisi  nchini kuharakisha zoezi la  kuanzisha na kuendesha Madawati ya Jinsia Katika Wilaya zote ili haki iweze kutendeka kwa wahanga wa ukatili wa jinsia wakiwemo watoto wa kike wanaokeketwa wangali wachanga.

Naibu Waziri huyo ametoa changamoto hiyo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kupinga ukeketaji duniani, iliyofanyika Kitaifa katika  kijiji cha Ngimu Wilayani Singida.

Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi amesema

Friday, February 14, 2014

Washtakiwa wanne huru kwenye tuhuma za kumuua Mwenyekiti wa UVCCM.

Washitakiwa watano wanaokabiliwa na shitaka la mauaji ya mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi Yohana Mpinga,wakisindikizwa na polisi kurejea mahabusu baada ya kesi yao kuahirishwa hadi vikao vingine vijavyo.Mahakama kuu iliwaachia washitakiwa huru wanne waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji hayo ya Mpinga baada mwendesha mashitakiwa kuwafutia mashitaka.

MAHAKAMA kuu kanda ya kati iliyoanza vikao vyake leo mjini Singida imewaachia huru washitakiwa wanne kati ya tisa waliokuwa wakikabiliwa na tuhuma ya kuuawa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi,Yohana Mpinga.

 Washitakiwa hao waliachiwa huru baada ya Mwendesha Mashitaka Mwanasheria wa serikali Caren Mrango,kudai mbele ya Jaji wa Mahakama kuu kanda ya kati,Cresentia Makuru kuwa Mwendesha Mashitaka mkuu hana nia ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao.

Aliwataja washitakiwa hao wanaotakiwa kuondolewa kwenye kesi hiyo kuwa ni Frank Stanley,Francis Edward,Tito Nintwa Kishogere na Paulo Nashokingwa.

Baada ya ombi hilo,jaji aliridhia ombi hilo na kuwaeleza washitakiwa kwamba pamoja na kuachiwa huru,wanaweza tena kushitakiwa au kuunganishwa na kesi hiyo,endapo kutakuwa na umuhimu wa kufanya hivyo.

Washitakiwa waliobakia kuendelea na kesi hiyo,ni Manase Daud,William Elia,Charles Leonard,Emmanuel Shila na Josia Israel.

Mwendesha Mashitaka, Mrango alidai mbele ya jaji Makuru kuwa mnamo julai 14 mwaka 2012 saa tisa alasiri huko katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi mkoa wa Singida,washitakiwa kwa pamoja walimuuawa Yohana Mpinga baada ya kumpiga na kumsababishia kifo.

Amesema siku ya tukio CHADEMA walikuwa wameandaa mkutano wa hadhara ambao kiongozi wa chama hicho Mwita Waitara na Dk.Kitila Mkumbo walikuwa wautumie katika kueneza sera za chama hicho.

Amesema viongozi hao walitumia fursa hiyo kutoa

Wajasirimali 40 wapata mafunzo ya usimamizi na uthibiti wa fedha.

Mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la Mother and Children of Central Tanzania (MCCT), Everline Lyimo akitoa nasaha zake kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo wanachama wa shiriki hilo ikiwemo usimamizi na uthibiti wa fedha.
Mwezeshaji Elihuruma Hema,akitoa mafunzo ya usimamizi na uthibiti wa fedha kwa wanachama 40 wa shirika lisilo la kiserikali la Mother and children of central Tanzania (MCCT).Mafunzo hayo yalifanyikia kwenye ukumbi wa mikutano wa hotel ya Stanley mjini.
Baadhi ya wanachama wa shirika lisilo la kiserikali la Mother and Children of Central Tanzania waliohudhuria mafunzo ya usimamizi na uthibiti wa fedha yaliyofanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Stanley mjini Singida.

WANACHAMA 40 wa shirika lisilo la kiserikali la Mother and Children of Central Tanzania (MCCT) la mkoa wa Singida wamehudhuria mafunzo ya usimamizi na uthibiti wa fedha kwa lengo wawe na uwezo mpana zaidi wa kuboresha shughuli zao za ujasiriamali.

Akizungumza na waandishi wa habari,  Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Elihuruma Hema amesema pia lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanachama hasa wanawake, kujua taratibu za fedha kitaalam ili ziwasaidie kuendesha shughuli zao kwa ufanisi.

Amesema katika kuwajengea uwezo wanachama hao,wamefundishwa namna bora ya kuweka kumbu kumbu za fedha kwenye vitabu husika ili mwisho wa siku iwe rahisi kwao kujua wanapata faida au hasara.

 ”Kwa ujumla maisha yanahitaji mahesabu, ukisimamia vizuri mahesabu ikiwemo ya biashara ni lazima faida itapatikana.  Lakini ukifanya tofauti ikiwemo kutokutumia vitabu husika katika kuweka kumbu kumbu ya fedha vizuri utapoteza fedha bila kujijua”,alifafanua Hema.

Mkufunzi huyo amesema kutokana na ukweli huo, kila mtu au mjasiriamali anapaswa kuhakikisha

Tuesday, February 11, 2014

Wawili wapoteza maisha katika ajali ya basi la Zuberi.

WASOMAJI WETU TUNAOMBA RADHI KAMA UTAKWAZIKA NA PICHA ZIFUATAZO.
Mtoto mmoja aliyelalaliwa na kusababisha kifo chake na basi la Zuberi T.119 AZZ lilokuwa likitokea Mwanza kuelekea jijini Dar-es-salaam na kupinduka katika eneo la kijiji cha Tumaini kata ya Issuna wilaya ya Ikungi wakati likimkwepa bibi aliyekuwa akikatisha barabara.
 Mmoja wa majeruhi akiwa amelazwa katika Hosptali ya Mkoa ya Singida.
 Mmoja wa majeruhi akiongea na waandishi wa habari katika Hospitali ya mkoa mjini Singida.

BASI la kampuni ya Zuberi T.119 AZZ lililokuwa linatokea jijini Mwanza likielekea jijini Dar-es-salaam,limepinduka na kusababisha vifo vya abiria  wawili na kujeruhi vibaya wengine arobaini wakati likimkwepa bibi mmoja aliyekuwa anakatisha barabara.

 Ajali hiyo imetokea jana saa 7.30 mchana katika barabara kuu ya Sindida –Dodoma eneo la kijiji cha Tumaini kata ya Issuna wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

Afisa wa makosa ya jinai mkoa wa Singida (RCO), Thobias Sedoyeka amesema kuwa basi hilo lililokuwa likiendeshwa na Fadhili Kalembo (35),lilipofika eneo la tukio,bibi mmoja alijitokeza akiwa anavuka barabara.

Amesema dereva wa basi alijitahidi kumkwepa bibi huyo lakini ghafla bibi alirudi tena barabarani kitendo kilichosababisha basi hilo kupinduka na kuserereka hatua zaidi ya 50 wakati likimkwepa kwa mara ya pili.

 “Basi hili lilimlalia mtoto mdogo ambaye

DC akemea posho kwa viongozi wa umma.

Mkuu wa wilaya ya Singida, Mwalimu Queen Mwashinga Mlozi, akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa mrejesho wa utafiti wa marejesho ya taarifa ya mradi wa ufuatiliaji na uwajibikaji jamii.Wa kwanza kulia,ni kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Singida na afisa biashara wa halmashauri hiyo,Shao.Wa kwanza kushoto ni Afisa kutoka shirika la HAPA.
Afisa mwanadamizi wa shirika lisilo la kiserikali la Health Actions Promotion Assocition (HAPA) la mkoa wa Singida, Mnyambi akitoa nasaha zake muda mfupi kabla hajamkaribisha mkuu wa wilaya ya Singida Queen Mlozi, kufungua mkutano wa mrejesho wa utafiti juu ya uwajibikaji.Wa kwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi.
Afisa wa shirika la HAPA, Baraka Mwakubali akitoa taarifa yake ya marejesho ya taarifa ya mradi wa ufuatiliaji na uwajibikaji jamii kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa katoliki mjini Singida.
Baadhi wa wajumbe waliohudhuria mkutano wa marejesho ya taarifa ya mradi wa ufuatiliaji na uwajibikaji jamii.Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa katoliki mjini Singida

MKUU wa Wilaya ya Singida Queen Mlozi ameonya viongozi wanaoweka tamaa mbele ya malipo ya posho wasithubutu kuchukua fomu za kuomba uongozi wowote kwa madai kwamba katika kuwatumikia wananchi, posho sio kipaumbele.

Mlozi ametoa onyo hilo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye mkutano wa  marejesho wa taarifa ya mradi wa ufuatiliaji na uwajibikaji jamii uliofanyika kwenye ukumbi wa mkutano wa Kanisa Katoliki mjini hapa.

Amesema kazi nyingi za kuwatumikia wannchi ni za kujitolea kwa hali hiyo kiongozi anayetaka kulipwa posho, huyo hafai kwa sababu atadumaza maendeleo

“Kama unaona huwezi kufanya kazi za wanachi bila kulipwa posho basi usichukue fomu ya kuomba uongozi kwa sababu utakuwa kikwazo kwa maendeleo ya wananchi”.

Awali afisa wa shirika la uboreshaji afya ya jamii (HAPA) Baraka Mwakubali, amesema lengo la ufuatiliaji na uwajibikaji  jamii, ni kuboresha  mfumo wa

Tanesco kutumia shilingi 48 bilioni kusambaza Umeme Vijijini Singida.

Meneja wa TANESCO mkoa wa Singida, Maclean Mbonile akiwa ofisini kwake kutekeleza majukumu yake ya kila siku.

SHIRIKA la umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa singida linatarajia kutumia zaidi ya shs. 48.3 bilioni kugharamiwa awamu mbili za miradi ya usambazaji umeme vijijini chini ya mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN).

Akizungumuza na waandishi wa habari ofisini kwake hivi karibun, Meneja wa TANESCO mkoa wa singida, Maclean Mbonile amesema miradi yote inafadhiliwa na wakala wa nishati vijijini (REA ).

Amesema awamu ya kwanza utekelezaji wake ilianza julai 2010 na kukamilika mwishoni mwa Septemba mwaka jana. Awamu hiyo imegharimu  dola za kimarekani 9.94 milioni.

Amesema awamu ya pili imeanza kutekeleza mapema oktomba jana (2013), na inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24. Awamu hii ya pili, inakadiriwa kugharimu jumla ya dola za kimarekani 20 milioni.

Mbonile amesema utekelezaji wa miradi hiyo, unasimamiwa na TANESCO  pamoja na uongozi wa serikali ya mkoa wa Singida .Ujenzi wake unafanywa na mkadarasi  binafsi aliyeshinda zabuni  M/S Spencon Services Ltd.

“Awamu ya kwanza tumeweza kuwapatia huduma ya umeme wananchi /wateja

Wednesday, February 5, 2014

Matembezi ya mshikamano ya CCM manispaa ya Singida.

Baadhi ya wanachama wa CCM manispaa ya Singida,wakishiriki matembezi ya mshikamano ya kilomita kumi ikiwa ni sehemu ya sherehe ya maadhimisho ya CCM kutimiza miaka 37 toka kianzishwe.
Katibu wa CCM mkoa wa Singida,Naomi Kampambala ( mstari wa pili wa kwanza kulia mwenye kofia kapelo) akijumuika na wanaCCM wa manispaa ya Singida,kwenye matembezi ya mshikamano yaliyofanyika jana ya kilomita kumi.

Mstahiki meya wa halmashauri ya manispaa ya Singida na sheikh wa mkoa wa Singida,Sheikh Salum Mahami,(wa pili kushoto) akishiriki matembezi ya kilomita kumi ya mshikamano ya CCM .

Shirika lisilo la Kiserikali latumia zaidi ya shilingi 562 milioni kugharamia sekta ya maji na usafi wa mazingira

Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Health Actions Promotion Association (HAPA) la mjini Singida, David Mkanje, akiwa ofisini kwake akitekeleza majukumu yake.

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Health Action Promotion Association (HAPA) la mkoani hapa limetumia zaidi ya shilingi 562 milioni kugharamia sekta ya maji na usafi wa mazingira katika mkoa wa Singida na Morogoro.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na mkurugenzi wa HAPA,David Mnkaje wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi katika kipindi cha kuanzia januari hadi desemba mwaka jana.

Amesema kati ya fedha hizo,zimetumika kwenye ujenzi wa vyoo bora na vya kisasa katika shule za msingi tano wilayani Iramba.Shule hizo zilizonufaika na mradi huo ni Dominiki,Midimbwi,Munguli,Nyahaa na Lugongo.

Aidha,Mnkeje amesema kupitia projecti ya WFP,wamejenga matenki 48 ya kuvunia maji ya mvua katika baadhi ya shule za msingi zilizopo wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga,Kondoa (Dodoma),Iramba,Singida vijijini na Ikungi zote za mkoa wa Singida.

“Pia katika mwaka uliopita,tumeweza kujenga zahanati na kusaidia baadhi ya vitendea kazi katika vijiji vya Kinampundu na Milade vya wilaya ya Mkalama.Kazi hii ya kujivunia,tumesaidina na vijana wa kujitolea (volunteers) kutoka nje ya nchi (ulaya) na wakazi wa vijiji husika”,amesema Mnkeje kwa kujiamini.

Katika hatua nyingine,Mkurugenzi huyo amesema kupitia project nyingine iliyofadhiliwa na Care,alisema kujenga vyoo bora kabisa katika shule za msingi za Mkundi,Chaumbele na Madege vya wilaya ya Mvomero katika mkoa wa Morogoro.Shule hizo pia zilijengewa matanki ya kuvunia maji ya mvua.

“Kwa mkoa wa Morogoro,kupitia mradi mwingine wa WADA,tumeweza kujenga

Shirika lisilo la kiserikali toka Uingereza lakabidhi vifaa vya thamani Tsh 20m kwa mafundi wadogo.

Katibu tawala mkoa wa Singida, Hassan Liana, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa kwa mafundi wadogo wa useremala,ushonaji wa nguo,uhunzi na ujenzi.Vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 20 milioni,vimetolewa na shirika la Tools for self reliance la nchini Wales Uingereza na zimepitia SIDO mkoa wa Singida.


Katibu tawala mkoa wa Singida, Hassan Liana (wa pili kulia) akikabidhi cherehani kwa mmoja wa kiongozi wa vikundi 17 vilivyonufaika na msaada wa vifaa vya ufundi vilivyotolewa na shirika la Tools for self reliance la nchini Wales Uingereza.Wa kwanza kulia ni meneja wa SIDO mkoa wa Singida, Shoma Kibende.
Katibu tawala mkoa wa Singida, Hassan Liana, akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa vikundi 17 vya mafundi wa fani mbalimbali muda mfupi baada ya kuwakabidhi vifaa vya ufundi vilivyotolewa na shirika la Tools for self reliance la nchini Wales Uingereza.Wa kwanza kushoto ni mejena wa SIDO mkoa wa Singida, ndugu Shoma Kibende.

Wakazi wa kanda ya kati waomba kutoa taarifa sahihi ya nguvu kazi ya Taifa.

Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi, akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili ya wadadisi na wahariri wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi katika mikoa ya Singida ,Dodoma, Tabora na Kigoma.Mafunzo hayo yanafanyikia kwenye ukumbi wa mikutano wa VETA mjini Singida.
Baadhi ya wadadisi na wahariri wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi katika mikoa ya Kigoma, Tabora, Singida na Dodoma wakiwa kwenye mafunzo ya wiki mbili yanayohusu utafiti huo unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.
Mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadadisi na wahariri wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi katika mikoa ya Singida,Kigoma,Tabora na Dodoma na wakufunzi wao.

MKUU  wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone amewataka wakazi wa kanda ya kati kutoa taarifa sahihi kwa wadadisi na wahariri wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi ili serikali iweze kutambua hali halisi ya ajira nchini.

Dr. Kone ametoa wito huo hivi karibuni wakati akifungua mafunzo ya wadadisi na wahariri wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2014.

Amesema utafiti huo ambao mahojiano yake yanatarajiwa kufanywa katika kaya 11,520 nchini, unatarajiwa kuanza mapema mwezi ujao wa februari.

Dk. Kone amesema utafiti huo wa nguvu kazi nchini, utatoa viashiria muhimu ikiwemo kujua hali ya ajira nchini katika sekta rasmi na isiyo rasmi.

“Pia utatusaidia kujua kiwango cha ukosefu wa ajira, kiwango cha ajira isiyo timilifu, ajira mbaya, ajira hatarishi kwa watoto, hali ya kipato kutokana na ajira, matumizi ya muda na ajira mpya zilizozalishwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006/ hadi 2013”,amesema.

Aidha Mkuu huyo wa mkoa katika hotuba yake ilisomwa kwa niaba yake na DC wa Singida, Queen Mlozi, amewahakikishia wananchi kwamba taarifa watakazotoa zitakuwa ni za siri na zitatumika tu kwa matumizi ya kitakwimu pekee.

Kutokana na umuhimu wa utafiti huo, Dk. Kone amewahimiza wananchi wa mikoa ya Singida, Dodoma, Tabora na Kigoma kutoa

Shirika lisilo la kiserikali latumia shilingi 1.5 bilioni kwenye miradi

Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Health Actions Promotion Association (HAPA) la mjini Singida,David Mkanje akiwa ofisini kwake akitekeleza majukumu yake.

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Health Actions Promotion Association (HAPA) limetumia zaidi ya shilingi 1.5 bilioni katika kutekeleza miradi miwili mkoani hapa katika kipindi cha kuanzia janauari hadi desemba mwaka jana.

Miradi hiyo ni wa ushiriki sawa wa wanaume katika afya ya uzazi na jinsia (TMEP), uliofadhiliwa na shirika la RFSU la nchini Sweden kwa zaidi ya shilingi bilioni moja.

Mradi mwingine ni ule wa Pamoja Tunaweza (UFBR) ambao umefadhiliwa na shirika la SIMAVI la nchini Uholanzi, kwa kiasi cha shilingi milioni mia tano.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkurugenzi wa HAPA,David Mkanje alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake juu ya shughuli zilizofanywa na shirika hilo kongwe, kwa kipindi cha mwaka jana.

Kuhusu mradi wa ushiriki sawa wa wanaume katika afya ya uzani na jinsia,Mkanje amesema kuwa kata 21 za wilaya ya Manyoni,zimenufaika na maradi huo.

“Kwa upande wa manispaa ya Singida,jumla ya kata 13 ns Singida vijijini kata 28 nazo zimenufaika na mradi huo”,amesema na kuongeza kwa kusema;

“Mradi huu ni wa uhamasishaji kuhusu masuala ya afya ya uzazi na jinsia,ambapo wanaume wanalengwa kuwa chachu ya mabadiliko katika kuhakikisha matatizo yatokanayo na uzazu,yanakwisha”alifafanua Mkurugenzi huyo.

Katika hatua nyingine,Mkanje amesema kuwa mradi wa Pamoja Tunaweza (UFBR), umetekelezwa kwenye wilaya ya

Chadema kuendelea kuwavua uanachama viongozi mamluki.

Baadhi ya wakazi wa mji wa Singida,wakipokea helkopta iliyombeba mwanasheria wa CHADEMA, Tundu Lissu,ambaye alihutubia kwenye uwanja wa Ukombozi mjini Singida.
Mwanasheria wa CHADEMA Tundu Lissu,akihutubia mamia ya wakazi wa mji wa Singida katika operation ya kuimarisha chama hicho.Mkutano huo ulifanyika katika uwanja vya Ukombozi mjini Singida.

Baadhi wa wakazi wa Singida mjini,wakimsikiliza mwanasheria wa CHADEMA Tundu Lissu, wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Ukombozi mjini Singida.

MWENYEKITI wa Baraza la Vijana Taifa (BAVITA), John Heche amesema Chadema kitaendelea kuwavua uanachama kiongozi au mwanachama  yeyote, pindi anapobainika kusaliti ustawi wa chama hicho.

Heche aliyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa ukombozi mjini hapa.

Amesema CHADEMA kamwe haitawalea wasaliti kama CCM ambayo inalea mafisadi na mawaziri mizigo,itaendelea kuwavua uanachama wasaliti bila kujali umaarufu wa mtu au kiongozi.

 “Kelele zimepingwa sana kwamba CHADEMA sasa kinakufa kisa eti Zitto Kabwe,amevuliwa nafasi zake zote za uongozi.Wanasingida,hivi kweli CHADEMA ife kwa sababu ya mtu mmoja tu.Haitatokea kabisa”,amesema na kuongeza;

 “Viongozi wote mashuhuri hivi sasa kwenye chama cha CHADEMA,hata wakiondoka,chama kitabaki pale pale na hakitaterereka.Hakuna kiongozi au mwanachama ambaye yupo juu ya CHADEMA,kwa hiyo sisi viongozi tutaondoka,lakini CHADEMA itabaki pale pale”,alisisitiza Mwenyekiti huyo.

Heche amesema CHADEMA ikichukua dola,haitawalinda mafisadi au viongozi mizigo kama inavyofanya CCM,CHADEMA itawafukizia mbali na endapo kutakuwa na adhabu ya kuwanyonga hadi wafe,adhabu hiyo itatekelezwa bila ubishi.

Kwa upande wake Mwanasheria wa CHADEMA,Tundu Lissu amewataka Watanzania mwakani (2015),kuchagua