Sunday, February 16, 2014

Jeshi la Polisi lahimizwa kuendesha kwa ufanisi madawati ya jinsia ili haki itendeke.

Mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi akisoma hotuba ya Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Jasmine Kairuki kwenye kilele cha maadhimisho ya kupinga ukeketaji duniani yaliyofanyika kitaifa ijiji cha Ngimu wilaya ya Singida.Wa kwanza kushoto,ni mwakilishi wa jumuiya ya kikiristo Tanzania (CCT),Mary Shuma.
Mwakilishii wa jumuiya ya kikiristo Tanzania (CCT), Mary Shuma, akitoa taarifa yake kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji duniani yaliyofanyika kitaifa katika kijiji cha Ngimu wilaya ya Singida.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Ngimu wilaya ya Singida,wakifuatailia matukio yaliyokuwa yakijiri kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kupinga ukeketaji duniani yaliyofanyika kitaifa katika kijiji cha Ngimu.

NAIBU Waziri wa Sheria na Katiba Angellah Jasmine Kairuki amelihimiza Jeshi la Polisi  nchini kuharakisha zoezi la  kuanzisha na kuendesha Madawati ya Jinsia Katika Wilaya zote ili haki iweze kutendeka kwa wahanga wa ukatili wa jinsia wakiwemo watoto wa kike wanaokeketwa wangali wachanga.

Naibu Waziri huyo ametoa changamoto hiyo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kupinga ukeketaji duniani, iliyofanyika Kitaifa katika  kijiji cha Ngimu Wilayani Singida.

Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi amesema
madawati hayo yakianzishwa hata katika kila kituo, yatasaidia  mno wahanga kupeleka malalamiko  yao juu ya kutendewa vitendo vya kikatili ambayo ni kinyume na haki za binadamu.

No comments:

Post a Comment