Tuesday, February 11, 2014

DC akemea posho kwa viongozi wa umma.

Mkuu wa wilaya ya Singida, Mwalimu Queen Mwashinga Mlozi, akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa mrejesho wa utafiti wa marejesho ya taarifa ya mradi wa ufuatiliaji na uwajibikaji jamii.Wa kwanza kulia,ni kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Singida na afisa biashara wa halmashauri hiyo,Shao.Wa kwanza kushoto ni Afisa kutoka shirika la HAPA.
Afisa mwanadamizi wa shirika lisilo la kiserikali la Health Actions Promotion Assocition (HAPA) la mkoa wa Singida, Mnyambi akitoa nasaha zake muda mfupi kabla hajamkaribisha mkuu wa wilaya ya Singida Queen Mlozi, kufungua mkutano wa mrejesho wa utafiti juu ya uwajibikaji.Wa kwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi.
Afisa wa shirika la HAPA, Baraka Mwakubali akitoa taarifa yake ya marejesho ya taarifa ya mradi wa ufuatiliaji na uwajibikaji jamii kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa katoliki mjini Singida.
Baadhi wa wajumbe waliohudhuria mkutano wa marejesho ya taarifa ya mradi wa ufuatiliaji na uwajibikaji jamii.Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa katoliki mjini Singida

MKUU wa Wilaya ya Singida Queen Mlozi ameonya viongozi wanaoweka tamaa mbele ya malipo ya posho wasithubutu kuchukua fomu za kuomba uongozi wowote kwa madai kwamba katika kuwatumikia wananchi, posho sio kipaumbele.

Mlozi ametoa onyo hilo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye mkutano wa  marejesho wa taarifa ya mradi wa ufuatiliaji na uwajibikaji jamii uliofanyika kwenye ukumbi wa mkutano wa Kanisa Katoliki mjini hapa.

Amesema kazi nyingi za kuwatumikia wannchi ni za kujitolea kwa hali hiyo kiongozi anayetaka kulipwa posho, huyo hafai kwa sababu atadumaza maendeleo

“Kama unaona huwezi kufanya kazi za wanachi bila kulipwa posho basi usichukue fomu ya kuomba uongozi kwa sababu utakuwa kikwazo kwa maendeleo ya wananchi”.

Awali afisa wa shirika la uboreshaji afya ya jamii (HAPA) Baraka Mwakubali, amesema lengo la ufuatiliaji na uwajibikaji  jamii, ni kuboresha  mfumo wa
usimamizi wa rasilimali za umma kwa kuwataka wananchi kujenga utamaduni wa kudai na kuhoji utendaji wa Serikali yao kuanzia Serikali za Vijiji.

Katika ufuatiliaji huo, amesema wabaini shilingi 9.6 milioni za ujenzi wa miundombinu ya uvunaji maji na kiasi kingine cha shilingi 44.4 milioni, zilizotolewa kwa ajili ya Ukarabati wa skimu ya maji Wilaya ya Singida, Hazikutolewa.

Akifafanua amesema  kuwa Serikali kaikutoa fedha hizo kwa madai kuwa baadhi ya wadau /wafadhili hawakuchangia fedha katika miradi mbalimbali mamendeleo.

Aidha Baraka alitowa fursa hiyo  kuipongeza  halmashauri ya Wilaya ya Singida, kwa jitihada zake za kutunga Sheria ndogo ndogo ni za vyanzo  vipya vya mapato ya ushuru na madai na minara ya simu .

“Pia naipongeza  halmashauri ya Singida kwa hatua yake  ya  kuunda timu  ya kukusanya  msapato ambayo  tarahisisha kusimamia na kufuatilia kwa njia elekezi na shirikishi.”

No comments:

Post a Comment