Friday, February 14, 2014

Washtakiwa wanne huru kwenye tuhuma za kumuua Mwenyekiti wa UVCCM.

Washitakiwa watano wanaokabiliwa na shitaka la mauaji ya mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi Yohana Mpinga,wakisindikizwa na polisi kurejea mahabusu baada ya kesi yao kuahirishwa hadi vikao vingine vijavyo.Mahakama kuu iliwaachia washitakiwa huru wanne waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji hayo ya Mpinga baada mwendesha mashitakiwa kuwafutia mashitaka.

MAHAKAMA kuu kanda ya kati iliyoanza vikao vyake leo mjini Singida imewaachia huru washitakiwa wanne kati ya tisa waliokuwa wakikabiliwa na tuhuma ya kuuawa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi,Yohana Mpinga.

 Washitakiwa hao waliachiwa huru baada ya Mwendesha Mashitaka Mwanasheria wa serikali Caren Mrango,kudai mbele ya Jaji wa Mahakama kuu kanda ya kati,Cresentia Makuru kuwa Mwendesha Mashitaka mkuu hana nia ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao.

Aliwataja washitakiwa hao wanaotakiwa kuondolewa kwenye kesi hiyo kuwa ni Frank Stanley,Francis Edward,Tito Nintwa Kishogere na Paulo Nashokingwa.

Baada ya ombi hilo,jaji aliridhia ombi hilo na kuwaeleza washitakiwa kwamba pamoja na kuachiwa huru,wanaweza tena kushitakiwa au kuunganishwa na kesi hiyo,endapo kutakuwa na umuhimu wa kufanya hivyo.

Washitakiwa waliobakia kuendelea na kesi hiyo,ni Manase Daud,William Elia,Charles Leonard,Emmanuel Shila na Josia Israel.

Mwendesha Mashitaka, Mrango alidai mbele ya jaji Makuru kuwa mnamo julai 14 mwaka 2012 saa tisa alasiri huko katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi mkoa wa Singida,washitakiwa kwa pamoja walimuuawa Yohana Mpinga baada ya kumpiga na kumsababishia kifo.

Amesema siku ya tukio CHADEMA walikuwa wameandaa mkutano wa hadhara ambao kiongozi wa chama hicho Mwita Waitara na Dk.Kitila Mkumbo walikuwa wautumie katika kueneza sera za chama hicho.

Amesema viongozi hao walitumia fursa hiyo kutoa
lugha ya matusi kwa mbunge wa jimbo hilo kitendo kilicho sababisha kutokea vurugu kati ya wafiasi wa CHADEMA na CCM.

“Vurugu hizo lisababisha marehemu Yohana kuanza kufukuzwa ili apigwe na aliweza kukimbia na kuingia ndani ya nyumba ya Chume Manase na kuuliwa humo”,alifafanua.

Amesema washitakiwa walipomaliza kazi ya kumuuawa Yohana,walirudi kwenye mkutano na kudai kwamba kazi tayari wameishaimaliza.


Washitakiwa hao watano wanaotetetewa na wakili wa kujitegemea kutoka Dodoma mjini Deus Nyabiri,walikana shitaka hilo na kurudishwa rumande hadi hapo vikao vingine vya mahakama kuu vitakavyofanyika mkoani Singida,

No comments:

Post a Comment