Tuesday, February 11, 2014

Tanesco kutumia shilingi 48 bilioni kusambaza Umeme Vijijini Singida.

Meneja wa TANESCO mkoa wa Singida, Maclean Mbonile akiwa ofisini kwake kutekeleza majukumu yake ya kila siku.

SHIRIKA la umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa singida linatarajia kutumia zaidi ya shs. 48.3 bilioni kugharamiwa awamu mbili za miradi ya usambazaji umeme vijijini chini ya mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN).

Akizungumuza na waandishi wa habari ofisini kwake hivi karibun, Meneja wa TANESCO mkoa wa singida, Maclean Mbonile amesema miradi yote inafadhiliwa na wakala wa nishati vijijini (REA ).

Amesema awamu ya kwanza utekelezaji wake ilianza julai 2010 na kukamilika mwishoni mwa Septemba mwaka jana. Awamu hiyo imegharimu  dola za kimarekani 9.94 milioni.

Amesema awamu ya pili imeanza kutekeleza mapema oktomba jana (2013), na inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24. Awamu hii ya pili, inakadiriwa kugharimu jumla ya dola za kimarekani 20 milioni.

Mbonile amesema utekelezaji wa miradi hiyo, unasimamiwa na TANESCO  pamoja na uongozi wa serikali ya mkoa wa Singida .Ujenzi wake unafanywa na mkadarasi  binafsi aliyeshinda zabuni  M/S Spencon Services Ltd.

“Awamu ya kwanza tumeweza kuwapatia huduma ya umeme wananchi /wateja
1,503 katika awamu ya pili tunataajia wananchi /wateja 8,526 wapatao huduma ya umeme katika vijiji vya mradi .Idadi hii ni sawa na ongezeko la asilimia 52 ya idadi ya wateja wote mkoani”,alifafanua Meneja Mbonile

Meneja huyo alitaja wilaya na idadi ya miradi ya umeme vijijini kwenye mabano kwani Manyoni (33) ,Mkalama(15) , Iramba ( 26 ) ,Manispaa ya singida (2), Ikungi ( 5) , na singida vijijini ( 9).


Mbonile alitumia fursa hiyo kuwahimiza wakazi wa maeneo ya miradi ya umeme vijijini kutoa ushirikiano wa dhati ili miradi hiyo iweze kukamilika katika kipindi kilichopangwa.

No comments:

Post a Comment