Wednesday, February 5, 2014

Wakazi wa kanda ya kati waomba kutoa taarifa sahihi ya nguvu kazi ya Taifa.

Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi, akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wiki mbili ya wadadisi na wahariri wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi katika mikoa ya Singida ,Dodoma, Tabora na Kigoma.Mafunzo hayo yanafanyikia kwenye ukumbi wa mikutano wa VETA mjini Singida.
Baadhi ya wadadisi na wahariri wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi katika mikoa ya Kigoma, Tabora, Singida na Dodoma wakiwa kwenye mafunzo ya wiki mbili yanayohusu utafiti huo unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.
Mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadadisi na wahariri wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi katika mikoa ya Singida,Kigoma,Tabora na Dodoma na wakufunzi wao.

MKUU  wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone amewataka wakazi wa kanda ya kati kutoa taarifa sahihi kwa wadadisi na wahariri wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi ili serikali iweze kutambua hali halisi ya ajira nchini.

Dr. Kone ametoa wito huo hivi karibuni wakati akifungua mafunzo ya wadadisi na wahariri wa utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2014.

Amesema utafiti huo ambao mahojiano yake yanatarajiwa kufanywa katika kaya 11,520 nchini, unatarajiwa kuanza mapema mwezi ujao wa februari.

Dk. Kone amesema utafiti huo wa nguvu kazi nchini, utatoa viashiria muhimu ikiwemo kujua hali ya ajira nchini katika sekta rasmi na isiyo rasmi.

“Pia utatusaidia kujua kiwango cha ukosefu wa ajira, kiwango cha ajira isiyo timilifu, ajira mbaya, ajira hatarishi kwa watoto, hali ya kipato kutokana na ajira, matumizi ya muda na ajira mpya zilizozalishwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006/ hadi 2013”,amesema.

Aidha Mkuu huyo wa mkoa katika hotuba yake ilisomwa kwa niaba yake na DC wa Singida, Queen Mlozi, amewahakikishia wananchi kwamba taarifa watakazotoa zitakuwa ni za siri na zitatumika tu kwa matumizi ya kitakwimu pekee.

Kutokana na umuhimu wa utafiti huo, Dk. Kone amewahimiza wananchi wa mikoa ya Singida, Dodoma, Tabora na Kigoma kutoa
ushirikiano kama walivyoutoa wakati wa zoezi la sense la watu na makazi agositi 2012.

Kwa mujibu wa Dk. KOne jumla ya ajira 610,285 zimepatikana nchini kutokanana uwekezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na uwekezajikatika sekta binafsi kati ya mwaka 2010 hadi mwaka jana.

No comments:

Post a Comment