Wednesday, February 5, 2014

Matembezi ya mshikamano ya CCM manispaa ya Singida.

Baadhi ya wanachama wa CCM manispaa ya Singida,wakishiriki matembezi ya mshikamano ya kilomita kumi ikiwa ni sehemu ya sherehe ya maadhimisho ya CCM kutimiza miaka 37 toka kianzishwe.
Katibu wa CCM mkoa wa Singida,Naomi Kampambala ( mstari wa pili wa kwanza kulia mwenye kofia kapelo) akijumuika na wanaCCM wa manispaa ya Singida,kwenye matembezi ya mshikamano yaliyofanyika jana ya kilomita kumi.

Mstahiki meya wa halmashauri ya manispaa ya Singida na sheikh wa mkoa wa Singida,Sheikh Salum Mahami,(wa pili kushoto) akishiriki matembezi ya kilomita kumi ya mshikamano ya CCM .
Wa kwanza kushoto ni katibu wa wazazi CCM mkoa wa Singida,Bwiga na watatu kushoto ni mjumbe wa halmashauri kuu (NEC) CCM taifa manispaa ya Singida,Hassan Mazala.

No comments:

Post a Comment