Tuesday, December 18, 2012

Waandishi 17 mkoani Singida wapatiwa mafunzo ya biashara na uchumi na kutakiwa kujiendeleza kielimu.

 Mkufunzi Mnaku Ambani akitoa mafunzo ya biashara na uchumi yaliyohudhuriwa na waandishi wa habari 17 wa mkoa wa Singida. Mafunzo hayo ya siku nne yalifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa katoliki mjini Singida.
Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Singida wakimsikiliza kwa makini mkufunzi Mnaku Ambani (hayupo kwenye picha) akitoa mada zake za biashara na uchumi.

 Wanachama wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Singida(Singpress), wamehimizwa kufanya juhudi za makusudi kumiliki ardhi ili pamoja na mambo mengine, kujijengea mazingira mazuri ya
kuboresha uchumi wao.
Wito huo umetolewa na mwezeshaji wa mafunzo ya biashara na uchumi Mnaku Ambani, yaliyohudhuriwa na waandishi wa habari 17 wa mkoa huu.
Amesema ardhi kwa sasa ni rasilimali ambayo mahitaji yake yanazidi kuongezeka kwa kasi kubwa, kutokana na hali hiyo, hata thamani yake nayo inazidi kuongezeka pia kwa kasi.
Katika hatua nyingine Ambani amewataka waandishi wa habari kuongeza kasi katika kujielimisha kwa bidii, iwe  kwa kwenda shule au kujisomea nyumbani.
Amesema mambo mengi sasa duniani yanabadilika kila kukicha yakiwemo ya teknolojia, kwa hiyo, ili kukabiliana na mabadiliko hayo,ni lazima mwandishi wa habari ujitume katika kujiendeleza kielimu.
Ambani amewataka wasiridhike na elimu waliyonayo na watambue kwamba bado wanayo safari ndefu ya kujielimisha ili waweze kwenda na wakati.
Mafunzo hayo ya siku nne yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa katoliki mjini Singida, yaliandaliwa na Singpress na kufadhiliwa na Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari (UTPCT) nchini wenye makazi yake jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment