Leo
mwenzetu na ndugu yetu dada Elikiza amepoteza uhai wake katika makutano
ya barabara ya Shekilango na Bagamoyo eneo la Bamaga wakati akitimiza
wajibu wake kama askari wa usalama barabarani kuyapanga na kutoa ishara
kwa magari ikizingatiwa leo kulikuwa na msafara wa mkuu wa nchi akiwa
katika kutimiza majukumu yake ya kila siku.
Si
yeye wala sisi hakuna aliyejua litakalotokea, kwani dakika chache kabla
alikuwa akitimiza wajibu wake kama ilivyo ada, lakini ghafla, alipatwa
na ajali ya kugongwa na gari iliyokuwa kasi, na kupelea kuanguka na
hatimaye kupoteza maisha akiwa katika eneo lake la kazi ambalo ni
barabarani.
Mashuhuda
wakiwa katika hali ya mshangao na majonzi walijongea kunako mwili wake
na kuufunika huku mengi yakizungumzwa kutokana na tukio hilo na pia watu
wakilijadili gari lililohusika.
Wana Singida Yetu Blog tunatoa pole kwa familia yake, ndugu, jamaa, marafiki, idara ya
usalama barabarani na watanzania wote kwa ujumla, hakuna aliyetegemea
kwamba dada yetu sasa hizi hatutakuwa naye tena.
Maisha ndivyo yalivyo lolote laweza kutokea popote. Poleni watanzania.
Ee Mola ipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi Amin.
No comments:
Post a Comment