Diwani wa kata ya Unyamikumbi
Mosses Shaban Ikaku, akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa
manispaa ya Singid. Kikao hicho kilikuwa maalum kwa ajili ya kupitisha
bajeti ya manispaa ya Singida kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014.
Watendaji
wa halmashauri ya manispaa ya Singida wameshauriwa kujenga utamaduni wa
kusimamia kikamilifu misaada mbalimbali inayotolewa na mbunge wa jimbo
la Singida mjini Mh. Mohammed Dewji, ikiwemo ya sekta ya kilimo ili
manispaa hiyo iweze kupaa kimaendeleo.
Rai
hiyo imetolewa na diwani (CCM) kata ya Unyamikumbi Moses Shaban Ikaku,
wakati akizungumza kwenye kikao maalum cha madiwani ambacho kilipitisha
bajeti ya manispaa ya Singida kwa kipindi cha 2013/2014.
Amesema
misaada mingi na mikubwa inayotolewa na mbunge Dewji yenye lengo la
kuwapatia wananchi maendeleo endelevu, haijafikia malengo
yanayokusudiwa.
Moses
amesema kwa utafiti na uzoefu wake, miradi hiyo imekuwa haitoi matunda
mazuri kutokana na sababu kuu moja, nayo ni watendaji/wataalam
kutoisimamia kikamilifu.
Diwani
huyo meisema mfano hai na mzuri, ni wa msaada wa hivi karibuni wa
majembe ya kukokotwa na ng’ombe zaidi ya 500 na zaidi ya tani 60 za
mbegu bora za dengu, choroko na mbaazi.
Moses
amesema msaada huo wenye thamani kubwa na ambao ulikuwa na sharti nafuu
ambalo ni wakulima 10 kujiunga kwenye kikundi, kama ungesimamiwa
kikamilifu na wataalam wa kilimo na watendaji wengine, ungewakomboa
kiuchumi wakazi wa jimbo la Singida mjini.
Aidha,
amesema endapo majembe hayo yangetumika ipasavyo, ingechangia wakulima
kulima kisasa na kupanua ukubwa wa mashamba yao, kitendo ambacho
kigesaidia wakulima kupata mapato makubwa na kupelekea kununua trekta
kubwa.
“Nachukua
fursa hii kumshukuru na kumpongeza mbuge wangu Mh. Dewji , kwa kugawa
majembe zaidi ya 500 ya kukokotwa na wanyama kazi, lengo lake ni zuri
mno, kwa sababu analenga kusaidiana na serikali katika kufikia malengo
ya kilimo kwanza. Lakini nasikitika sana, kusema msaada huu huenda
usizae matunda mazuri kwa sababu hausimamiwi kikamilifu na wataalam wa
kilimo na watendaji wengine”amesema Moses kwa masikitiko.
Amesema
msaada huo na mingine mingi inayotolewa na Mh. Dewji, imekuwa kama ni
kiini macho mbele ya wataalam na watendaji wa manispaa, na kwa sababu
hiyo, imekuwa haifikii lengo.
Moses
amesema wakilitambua hilo na wakasimamia misaada inayotolewa kwa
wananchi ipasavyo, misaada hiyo itakuwa na tija zaidi kwa maana kwamba
itasaidia kupaisha maendeleo ya wananchi.
Pia
kwa njia hiyo, itamvutia zaidi mbunge Dewji na wadau wengine kuongeza
misaada zaidi ambayo itawakwamua wananchi kutoka kwenye lindi la
umaskini.
No comments:
Post a Comment