Mkuu wa mkoa wa Singida
Dk.Parseko Vicent Kone akifungua kikao cha 34 cha bodi ya barabara mkoa
wa Singida leo. Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa
ofisi ya mkuu wa mkoa mjini Singida.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha 34 cha bodi ya barabara mkoa wa Singida, wakifuatilia kwa makini kikao hicho kilichokuwa chini ya mwenyekiti ambaye ni mkuu wa mkoa wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Vicent Kone (hayupo kwenye picha).
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha 34 cha bodi ya barabara mkoa wa Singida, wakifuatilia kwa makini kikao hicho kilichokuwa chini ya mwenyekiti ambaye ni mkuu wa mkoa wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Vicent Kone (hayupo kwenye picha).
Mkuu
wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Vicent Kone ameuagiza wakala wa barabara
(TANROADS), kusimamia kwa karibu na kuhakikisha wakandarasi wanaopewa
kazi ya kujenga barabara, wanajenga kwa viwango vilivyoainishwa kwenye
mikataba yao.
Dk. Kone amesema kwa njia hiyo kutasaidia mno kupunguza mianya ya kupoteza fedha za umma na pia, kuondoa malalamiko kutoka kwa viongozi na wananchi, kwamba ujenzi husika haufanani na fedha zilizotumika.
Mkuu
huyo wa mkoa ametoa agizo hilo leo wakati akifungua
kikao cha 34 cha
bodi ya barabara cha mkoa wa Singida, kilichofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini Singida.
Amesema
kumekuwa na malalamiko mengi ambayo yanaelekezwa kwa wajenzi wa
madaraja, makalvati na barabara, kuwa miundo mbinu hiyo inajengwa kwa
ubora usioridhisha kabisa.
Dk.
Kone amefafanua kuwa inawezekana mimi kama kiongozi au mwananchi yeyote
asiwe na elimu ya uhandisi, lakini akawa na ufahamu unaomuwezesha
kubaini kuwa barabara au daraja fulani, limejengwa chini ya kiwango,
hivyo tuheshimu maelekezo ya viongozi na kuwasikiliza wananchi, ili kazi
zetu ziwe na ubora unaotakiwa.
Katika
hatua nyingine, mkuu huyo wa mkoa amewataka wakurugenzi wa halmashauri
na mstahiki meya wa manispaa ya Singida kupitia mabaraza ya madiwani,
wasimamie kwa karibu ujenzi wa barabara zao, ili kutumia fedha kwa
thamani inayokusudiwa (value for money) na kuondokana na malalamiko
kutoka kwa wananchi ambao ndio walipa kodi.
Aidha,
Dk.Kone amewataka wakurugenzi hao na mstahiki meya, kutumia maabara za
TANROADS kwa ajili ya kupima ubora wa kazi zinazofanywa na wakandarasi.
Amesema upimaji huo ujumuishe pia na kupima ubora wa udongo uliotumika, uimara wa madaraja na makalvati yanayojengwa.
“Vile vile ameomba sana, tusikimbilie kuwalipa wakandarasi kabla hatujajiridhisha na kazi zao”amesema mkuu huyo wa mkoa.
Wakati
huo huo Dk.Kone ametumia fursa hiyo kuipongeza serikali kwa kumuamuru
mkandarasi CHICCO na mhandisi mshauri BCOM kutoka Ufaransa, kukijenga
upya kwa kiwango cha lami kipande cha barabara kati ya Sekenke na Shelui
chenye urefu wakilomita 33.3 kwa gharama zao.
Hii ni baada ya kubainika kuwa kipande hicho kilijengwa chini ya kiwango.
No comments:
Post a Comment