Mwalimu mkuu msaidizi wa
walemavu katika shule ya msingi mchanganyiko Ikungi wilaya ya Ikungi
mkoa wa Singida, Donard Bilali akitoa wito wake kwa rais Kikwete
kuangalia uwezekano wa kuteua walemavu kushika nafasi za ukuu wa
wilaya,mkoa na uwaziri kama anavyofanya kwa kundi la wanawake.
Mwalimu wa walemavu katika shule ya msingi mchanganyiko Ikungi wilayani Ikungi,Manase Ligula akitoa wapendekezo yake kuwa katiba ijayo,iagize wamiliki wa vyombo vya usafiri,watoe huduma bure kwa walemavu.
Mwalimu wa walemavu katika shule ya msingi mchanganyiko Ikungi wilayani Ikungi,Manase Ligula akitoa wapendekezo yake kuwa katiba ijayo,iagize wamiliki wa vyombo vya usafiri,watoe huduma bure kwa walemavu.
Rais
wa jamhuri ya muungano Tanzania,Dk.Jakaya Mrisho Kikwete ameshauriwa
kuangalia uwezekano wa kuteua walemavu kushika nafasi za ukuu wa
wilaya,mkoa na uwaziri kwa wale wenye uwezo na sifa za kuongoza katika
nafasi hizo kwa ufanisi.
Wito
huo umetolewa na mwalimu mkuu msaidizi wa walemavu katika shule ya
msingi mchanganyiko ya Ikungi wilaya ya Ikungi , Donard Bilali wakati
akizungumza na Singida Yetu Blog juu ya zoezi la uundwaji wa mabaraza
ya katiba.
Amesema
serikali ya awamu ya nne iliyoko chini ya rais Kikwete,imefanya
mambo
mengi mazuri ikiwemo kushirikisha kikamilifu makundi mbalimbali ya watu
katika utendaji wa serikali.
“Kwa
moyo wa dhati kabisa,nampongeza sana rais Kikwete kwa hili la
ushirikishwaji,amefanya vizuri sana kwa kundi la wanawake.Sasa nadhani
wakati umefika na sisi walemavu atuangalie katika nafas za ukuu wa
wilaya,mkoa na hata uwaziri”,amesema mwalimu Bilali kwa kujiamini.
Mwalimu
Bilali ambaye pia ni katibu mkuu wa chama cha walemavu wilaya ya
Ikungi,alisema hata hivyo asiteue tu mtu mradi mlemavu, aangalie sifa,
uadilifu na uwezo wa kumudu nafasi husika.
Aidha
ameiomba serikali iwape haki sawa na watu wasio walemavu katika
kunufaika na mifuko mbalimbali ya umma ikiwemo fedha za JK,i li kundi
hilo liweze kupiga hatua katika kuboresha hali zao za kiuchumi.
Mwalimu
huyo ambaye ana ulemavu wa kutokuona, alipendekeza katiba ijayo
ibainishe wazi kuwa walemavu wasome bure kuanzia shule ya msingi hadi
chuo kikuu,kama njia mojawapo ya kuwavutia walemavu kujiendeleza
kielimu.
Kwa
upande wake mwalimu Manase Ligula,amesema upo umuhimu mkubwa kwa
walemavu wakajumuishwa kwenye mabara ya katiba, kwa madai kuwa wao ndio
wanaoyafahamu kwa kina mahitaji yao.
Mwalimu
Ligula ambaye ni mlemavu wa macho,alisema pia katiba ijayo iweke wazi
kuwa walemavu waruhusiwe na wamiliki wa vyombo vya usafiri kusafiri bure
popote aendapo.
Alisema
hilo linawezekana kwa madai kuwa kundi la walemavu ni dogo sana kwa
hali hiyo, litakuwa halina madhara yo yote kwa wamiliki wa vyombo vya
usafiri.
No comments:
Post a Comment