Katibu tawala wa wilaya ya
Iramba,Yahaya Naniya akizundua mradi wa maji wa kijiji cha Ntwike tarafa
ya Shelui uliogharimu zaidi ya shilingi 190 milioni.
Mhandishi wa idara ya maji wilaya ya Iramba akitoa taarifa yake kwenye kilele cha wiki ya maji iliyofanyika kiwilaya katika kijiji cha Ntwike wilaya ya Iramba.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Ntwike tarafa ya Shelui waliohudhuria maadhimisho ya wiki ya maji kiwilaya yaliyofanyikia kwenye kijiji hicho.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Nkokilangi tarafa ya Shelui wilaya ya Iramba,wakichota maji juzi kwenye mto wa durumo juzi.Hata hivyo,maji hayo si salama kwa afya ya binadamu.

Shirika
lisilo la kiserikali la mpango endelevu na uboreshaji mazingira
(SEMA), kwa kushirikiana na halmashuari ya wilaya ya Iramba na wananchi
wa kijiji cha Ntwike jimbo la Iramba Magharibi, kwa pamoja wamechangia
zaidi ya shilingi milioni 190.5 kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa mradi
wa maji katika kijiji cha Ntwike tarafa ya Shelui.
Afisa
mipango wa SEMA Hudson Kazonta amesema hayo wakati akizungumza kwenye
hafla ya uzinduzi wa mradi huo wa maji ambao ulikuwa ni
sehemu ya kilele
cha maadhimisho ya wiki ya maji duniani iliyofanyika kiwilaya katika
kijiji cha Ntwike.
Amesema
kati ya fedha hizo, shirika la Water Aid, kupitia SEMA, lilitoa zaidi
ya shilingi 152.2 milioni kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa mradi
huo wa maji.
Kazonta
amesema halmashauri ya wilaya ya Iramba, imechangia zaidi ya shilingi
30.5, milioni na wananchi kwa upande wao, wamechangia zaidi ya shilingi
15.2 milioni.
Afisa
huyo ametaja baadhi ya shughuli zilizofanyika kwenye mradi huo, kuwa ni
pamoja na kuchimba kisima kimoja kirefu, kujenga tanki lenye ujazo wa
lita 50,000 ,nyumba ya mashine ya maji na vituo tisa vya kuchotea maji.
Kwa mujibu wa Kazonta, mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka wa 2011/2012 na umekamilikaMei mwaka jana.
Kazonta
ametumia fursa hiyo, kuwataka wakazi wa kijiji cha Ntwike kuulinda na
kuutunza vizuri mradi huo wa maji ili uweze kutoa huduma kwa muda mrefu.
Kwa
upande wake Kaimu Mhandisi wa idara ya maji katika wilaya ya Iramba
Joel Kisubi, amesema wilaya hiyo ya Iramba yenye wakazi 414,219, wakazi
wake wanapata huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 46.
Aidha,
Joel amesema wilaya hiyo ina jumla ya vyanzo vya maji 699 vya aina
mbalimbali na kwamba 617 vinafanya kazi na vilivyobaki 82, havifanyi
kazi.
No comments:
Post a Comment