Bango la shule ya msingi mchanganyiko Ikungi wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi mchanganyiko Ikungi,wakiwa darasani.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi mchanganyiko Ikungi,wakiwa darasani.
Mwalimu mkuu wa shule ya
msingi mchanganyiko Ikungi wilaya ya Ikungi Olivary Kamilly akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo kwenywe picha) juu ya umuhimu wa walemavu
kushirikishwa kikamilifu katika uundaji wa mabaraza ya katiba.
Mwalimu
mkuu wa shule ya msingi mchanganyiko wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida
Olivary Kamilly, amependekeza walemavu washirikishwe kikamilifu katika
mabaraza ya katiba kwa madai kuwa ndio wenye uwezo mzuri wa kuwakilisha
mahitaji yao.
Mwalimu
Kamilly mwenye taaluma ya ufundishaji walemavu, ametoa pendekezo hilo
wakati akizungumza na Singida Yetu Blog ofisini kwake, juu ya uundaji
wa mabaraza ya katiba.
Amesema mahitaji ya walemavu yataelezwa vizuri zaidi na walemavu wenyewe kwa kuwa wanaishi na ulemavu.
Akifafanua
zaidi, mwalimu huyo mkuu amesema
sifa hiyo ya kuyajua kwa undani
mahitaji ya walemavu, hata mtaalamu yeyote wa watu wenye ulemavu au mtu
yeyote ambaye si mlemavu, hawezi kuwa na sifa ya kuyafahamu mahitaji
yote ya mlemavu.
Katika
hatua nyingine, mwalimu Kamilly amependekeza katiba ijayo ionyeshe wazi
nini kifanyike ili kuonyesha thamani ya utu wa watu wenye ulemavu.
Aidha,
amesema katiba ijayo itamke wazi nini kifanyike kwa wazazi/walezi wenye
tabia ya kuwaficha watoto wao wenye ulemavu badala ya kuwapeleka shule.
Mwalimu
Kamilly amesema katiba ya sasa ibara ya 12 kifungu 1-2, kinasema kuwa
binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa pia kila mtu anastahili
heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
Hata
hivyo, amesema ibara hiyo ipo kinadharia zaidi kuliko kiutendaji, kwani
walemavu wengi wanadharauliwa, wananyanyaswa na wanaonekana ni mzigo
katika jamii.
Shule
ya msingi mchanganyiko Ikungi mbali ya kuwa na wanafunzi wasio na
ulemavu, pia ina wanafunzi walio na mahitaji muhimu ambao ni wasioona
42, uoni hafifu 19, ulemavu wa ngozi (albino) 15 na ulemavu wa viungo
watano.
No comments:
Post a Comment