Serikali
ya mkoa wa Singida imesema tatizo la muda mrefu la uhaba wa maji kwa
wakazi wa Singida mjini, litakuwa historia ifikapo mwishoni mwa mwezi
ujao, baada ya mradi mkubwa wa maji unaofadhiliwa na benki ya kiarabu
(BADEA) na shirika la mafuta ulimwenguni (OPEC) utakapomalizika.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa wiki ya maji uliofanyika katika eneo la Irao,
halmashauri ya manispaa ya Singida, Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko
Vicent Kone akifafanua, amesema kuwa utekelezaji wa mradi huu, umefikia
kiwango cha aslimia 93 na unategemewa ifikapo
Aprili 30 mwaka huu,
utakuwa umekamilika.
Amesema
mwishoni mwa mwezi ujao,maji safi na salama yatakapitana kwa asilimia
mia moja, hii ni neema kubwa mno ambayo serikali ya awamu ya nne
inawapatia wakazi wa mji wa Singida.
Katika
hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na mkuu wa wilaya ya Singida
Mwalimu Queen Mlozi, mkuu huyo wa mkoa amewataka wakazi wa mji wa
Singida,kujenga kuwa na mwamko wa kulipa ankara zao za maji, kama njia
moja wapo ya kuishukuru serikali kwa kuwaondolea matatizo ya upatikanaji
wa maji.
“Pia
nawaombeni sana mjenge utamaduni wa kuwafichua watu wanaojiunganishia
maji kiholela, , kuchepusha dira za maji na wanaofanya uharibifu wa
miundo mbinu ya maji ikiwemo mabomba” amesema.
Awali
Meneja biashara wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Singida
mjini (SUWASA), Hosea Maghimbi, alisema madhumuni ya wiki hiyo ya maji
ni pamoja na kutoa fursa kwa wananchi kuielewa kikamilifu programu ya
maendeleo ya sekta ya maji ili waweze kushiriki utekelezaji wake.
Alitaja
madhumuni mengine kuwa ni kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi bora ya
maji, kuwaelimisha wananchi kuhusu utunzaji wa mazingira kwenye vyanzo
vya maji na kuwahamasisha wateja wake wa maji katika ulipaji wa ankra za
maji kwa wakati na kulipa malimbikizo ya madeni.
Kauli mbiu ya wiki ya maji kwa mwaka huu ni ‘mwaka wa ushirikiano wa maji kimataifa’.
No comments:
Post a Comment