Gari aina ya nissan presage axis C.6017 A, mali ya Abbakari Bakudikiza
(32) raia wa Rwanda baada ya kupata ajali kwenye kijiji cha Kisaki
manispaa ya Singida na kupelekea Abbakari kufariki dunia papo hapo. Gari
hilo lilikuwa likiendeshwa na mke wake raia wa Sweden Videl Ruze ambaye
alipata majeraha kichwani na amelazwa hospital ya mkoa na hali yake
inaendelea vizuri. Wanandoa hao ambao wameoana miezi sita iliyopita,
walikuwa wakitoa Dar-es-salaam kuelekea Rwanda.
Mwanaume
raia wa Rwanda Abbukari Bakudukiza (32) amefariki dunia hapo hapo,
baada ya gari walilokuwa wakisafiria na mke wake kupata ajali. Ajali
hiyo imetokea baada ya kupasuka tairi la mbele na kuacha njia na kisha
kupinduka.
Mke wa Abbakari raia wa Sweden ambaye alikuwa akiendesha gari hilo ni Videl Ruze (35).
Gari la familia hiyo ni Nissan presage axis C.6017 A.
Akizungumza
na Singida Yetu Blog mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida Dk. Suleiman
Muttani, amesema kuwa
ajali hiyo mbaya, imetokea katika eneo la kijiji
cha Kisaki manispaa ya Singida.
Amesema Abbakari amefariki kutokana na kuvunja damu nyingi baada ya kupata majeraha makubwa kichwani.
Dk.Muttani amesema Videl aliyekuwa akiendesha gari hilo yeye amepata
michumbuko sehemu za kichwani na amelazwa wodi namba tano, katika
hospitali ya mkoa mjini Singida na hali yake inaendelea vizuri, huku
mwili wa Abbakari ukihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha
hospitali ya mkoa.
Mkuu
wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi aliyemtembelea majeruhi Videl
wodini amesema kuwa majeruhi Videl amedai kuwa katika safari yao hiyo ya
kutoka Dar-es-salaam wakielekea Rwanda njiani walipata pancha mara
mbili.
“Majeruhi
huyo amesema kuwa wameoana na Mnyarwanda huyo miezi sita iliyopita na
kwa sasa ana mimba changa. Amedai walipoanza kuteremka mteremko wa
Kisaki, ndipo tairi la mbele lilipobasti na kupelekea kushindwa kulimudu
gari hilo”,alisema.
Mlozi
amesema kuwa tayari amekwisha wasiliana na ubalozi wa Rwanda nchini na
ndugu wa Abbakari wapo njiani kuja kuchukua mwili wa marehemu.
Kwa
upande wa mwanamke huyo kutoka Sweden, amesema pia amewasiliana na
ubalozi wa Sweden nchini na wao wanafanya utaratibu wa kuja kumwona
majeruhi huyo.
No comments:
Post a Comment