Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi (mbele ya basi lililopinduka aliyenyoosha mkono) akiangalia basi la Shabiby lililopinduka eneo la kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida.Basi hilo ambalo lilijeruhi abiria 28 akiwemo kondakta aliyevunjika miguu yote, lilipinduka katika harakati zake za kulipita basi jingine.
Lori la mafuta lililogongwa na basi la Shabiby na kusababisha abiria 28 kujeruhiwa.
Kondakta wa basi la shabiby Tadei Mhando aliyevunjika miguu yote miwili baada ya basi hilo kupinduka eneo la kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida. Waauguzi wa hospitali ya mkoa mjini hapa,wakimpeleka kondakta Tadei Mhando chumba cha upasuaji.
ABIRIA 48 wa basi la kampuni ya Shabiby lifanyalo safari zake kati ya mkoa wa Arusha na Dodoma, wamenusurika kufa baada ya basi hilo kupinduka wakati likijaribu kupita basi jingine.
Basi hilo aina ya Yutong lenye namba za usajili T.930 BUW, limepinduka katika barabara kuu ya Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Kisaki Manispaa ya Singida.
Ajali hiyo imetokea saa saba mchana wakati basi hilo likitokea mkoani Arusha kuelekea mjini Dodoma.
Kondakta wa basi hilo,Tadei Mhando amesema kati ya abiria hao,28 wakiwemo watoto wawili,wamepata majeraha katika sehemu zao mbalimbali za miili yao.
“Mimi ndiye niliyeumia zaidi kuliko majeruhi wote wa basi letu.Nimevunjika miguu yote miwili na sasa natarajia kuingizwa ‘theater’ kwa matibabu zaidi.Tunashukuru hakuna mtu aliyepoteza maisha”,amesema Tadei.
Akifafanua zaidi juu ya ajali hiyo,Tadei amesema walipofika eneo la tukio la Kisaki ambalo lina mwiinuko huku basi lao likiwa kwenye mwendo kasi,dereva wao alijaribu kulipita basi la Princess Muna.
Amesema katika jaribio hilo,mabasi yote mawili yakawa kwenye mwendo kasi unaofanana na wakati huo huo,
lori la mafuta lililokuwa linapishana na mabasi hayo,liliibana basi la shabiby na kusababisha ligonge lori hilo ubavuni karibu na kichwa.Basi hilo aina ya Yutong lenye namba za usajili T.930 BUW, limepinduka katika barabara kuu ya Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Kisaki Manispaa ya Singida.
Ajali hiyo imetokea saa saba mchana wakati basi hilo likitokea mkoani Arusha kuelekea mjini Dodoma.
Kondakta wa basi hilo,Tadei Mhando amesema kati ya abiria hao,28 wakiwemo watoto wawili,wamepata majeraha katika sehemu zao mbalimbali za miili yao.
“Mimi ndiye niliyeumia zaidi kuliko majeruhi wote wa basi letu.Nimevunjika miguu yote miwili na sasa natarajia kuingizwa ‘theater’ kwa matibabu zaidi.Tunashukuru hakuna mtu aliyepoteza maisha”,amesema Tadei.
Akifafanua zaidi juu ya ajali hiyo,Tadei amesema walipofika eneo la tukio la Kisaki ambalo lina mwiinuko huku basi lao likiwa kwenye mwendo kasi,dereva wao alijaribu kulipita basi la Princess Muna.
Amesema katika jaribio hilo,mabasi yote mawili yakawa kwenye mwendo kasi unaofanana na wakati huo huo,
“Kutokana na kubanwa huko, huku Shabiby likiwa kwenye mwendo kasi,dereva alishindwa kulimudu na hivyo kusababisha lipinduke na kuharibika vibaya”,alifafanua Tadei.
Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi na kamati yake ya ulinzi, ilifika hospital ya mkoa na kuwapa pole na majeruhi na kisha alienda eneo la tukio Kisaki.
No comments:
Post a Comment