Gari aina ya Noah T,730 BUX linavyoonekana baada ya kugongwa na Lori.
ABIRIA 13 wakiwemo watatu wa familia moja wamefariki dunia mkoani Singida leo, baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noah T.730 BUK, kugongwa na Lori aina ya Scania.
Ajali hiyo ya kusikitisha imetokea leo saa 1.32 asubuhi katika barabara kuu ya Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,SACP ,Geofrey Kamwela, amesema gari hilo aina ya Noah lilikuwa likitokea Itigi wilaya ya Manyoni na lilikuwa na safari ya kuja Singida mjini.
Amesema hadi sasa miili ya abiria 10 wamekwisha tambuliwa na ndugu zao na miili ya abiria watatu,bado haijatambuliwa na miili yote bado imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida
Alitaja waliotambuliwa na makazi yao kwenye mabano kuwa ni Omari Shaban (44) na mke wake Salma Omari na mtoto wao Nyamumwi Omari (10) wote wakazi wa Itigi mjini.
Kamwela alitaja wengine kuwa ni Haji Mohammed (29) (Msisi),Mtunku Rashidi (68) (Sajaranda),Salehe Hamisi (28) (Sajanranda),Samir Shaban (20) (Puma),Mwaleki Nkuwi (35) (Ikungi),Athumani Kalemba (38) na Ramadhan Mkenga (Sajaranda).Katika ajali hiyo,abiria watatu walinusurika na kupata majeraha madogo madogo.
Amefafanua juu ya ajali hiyo,Kamanda huyo alisema kuwa lori aina ya scania T.687 AXB wakati likipishana na noah,lilihama upande wake na kuifuata noah ambayo ilikuwa upande wake wa kushoto,na kuligonga na kisha kuliburuza kati zaidi ya 15.
“Kwa sasa bado hatujajua chanzo cha ajali hiyo mbaya ingawa baadhi ya watu wanadai kuwa huenda
dereva wa lori alisisia na kusababisha lori hilo kuhama upande wake na kufuata noah.Uchuguzi utakapokamilika,tutatoa taarifa hiyo”,amesema.Ajali hiyo ya kusikitisha imetokea leo saa 1.32 asubuhi katika barabara kuu ya Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,SACP ,Geofrey Kamwela, amesema gari hilo aina ya Noah lilikuwa likitokea Itigi wilaya ya Manyoni na lilikuwa na safari ya kuja Singida mjini.
Amesema hadi sasa miili ya abiria 10 wamekwisha tambuliwa na ndugu zao na miili ya abiria watatu,bado haijatambuliwa na miili yote bado imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida
Alitaja waliotambuliwa na makazi yao kwenye mabano kuwa ni Omari Shaban (44) na mke wake Salma Omari na mtoto wao Nyamumwi Omari (10) wote wakazi wa Itigi mjini.
Kamwela alitaja wengine kuwa ni Haji Mohammed (29) (Msisi),Mtunku Rashidi (68) (Sajaranda),Salehe Hamisi (28) (Sajanranda),Samir Shaban (20) (Puma),Mwaleki Nkuwi (35) (Ikungi),Athumani Kalemba (38) na Ramadhan Mkenga (Sajaranda).Katika ajali hiyo,abiria watatu walinusurika na kupata majeraha madogo madogo.
Amefafanua juu ya ajali hiyo,Kamanda huyo alisema kuwa lori aina ya scania T.687 AXB wakati likipishana na noah,lilihama upande wake na kuifuata noah ambayo ilikuwa upande wake wa kushoto,na kuligonga na kisha kuliburuza kati zaidi ya 15.
“Kwa sasa bado hatujajua chanzo cha ajali hiyo mbaya ingawa baadhi ya watu wanadai kuwa huenda
Wakati huo huo,mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini Singida,Dk.Banuba Deogratius amekiri kupokea miili ya abiria hao 13 na kusema kati yao,watoto ni wawili.
No comments:
Post a Comment