Friday, January 10, 2014

Akamatwa na noti bandia zaidi ya shilingi 3.4milioni.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela.
 
JESHI la Polisi Mkoani Singida linamshikilia mfanyabiashara mmoja kwa tuhuma za kupatikana na noti bandia za shilingi 10,000 na 5,000 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3.4 milioni

 Mtuhumiwa huyo Toye Wagela (39) mkazi wa kijiji cha Mitale mkoa wa Kigoma amekamatwa juzi saa nane mchana wakati akijaribu kununua chakula kwenye hotel moja wilayani Manyoni Mkoa wa Singida.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela amesema kuwa baada ya mtuhumiwa kutoa moja ya noti hizo na kutiliwa shaka alianza kujaribu kukimbia kabla ya kukamatwa na wananchi.

 Amesema kuwa wananchi hao waliita polisi ambapo baada ya kupekuliwa kwenye mifuko ya suruali, mtuhumiwa alikutwa na noti 200 za shilingi 10,000 na nyingine 209 za shilingi 5,000.

 Kamanda Kamwela amesema wanaendelea kufanya uchunguzi wa kina na kuwatafuta washirika wengine wa uhalifu huo,kabla ya mtuhumiwa kupandishwa  kizimbani kujibu tuhuma ya kupatikana na noti bandia.

No comments:

Post a Comment