Monday, January 20, 2014

Diwani wa CCM mbaroni kwa kuchoma basi la Mtei.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela.

DIWANI wa kata ya Umyambwa tarafa ya Mungumaji Halmashauri ya Manispaa ya Singida,(CCM) Shaban Satu na watu wengine tisa,wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kuchoma moto basi la kampuni ya Mtei Express ya mjini Arusha.

Diwani huyo na wapiga kura wake,inadaiwa kulichoma moto basi hilo januari tisa mwaka huu saa moja na dakika moja barabara ya Singida-Arusha eneo la kijiji cha Kisasida manispaa ya Singida.

Watuhumiwa hao walifikia uamuzi huo kutokana na basi hilo T.742 ACU lililokuwa linaendeshwa na Dismas Ludovick, kugonga bodaboda T.368 BXZ iliyokuwa imepakia watu wanne wa familia moja.

Wanafamilia hao ambao walikuwa wakienda shamba,ni Tamili,Kassim na Hamza ambao ni watoto wa Shabani Bunku ambaye alikuwa akiendesha bodaboda hiyo.Watoto wote watatu walipoteza maisha na baba yao bado anaendelea na matibabu katika hospitali ya misioni ya Hydom mkoani Manyara.

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela,amekiri diwani huyo na wapiga kura wake
kukamatwa kwa tuhuma ya kuchoma moto basi la Mtei.Ameahidi kutoa taarifa zaidi kazi itakapomalizika.

Mwandishi wa wa Singida Yetu Blog alishuhudia watuhumiwa hao wakishushwa kutoka gari la polisi kwenye kituo cha kati cha polisi mjini hapa.

No comments:

Post a Comment