Thursday, January 9, 2014

Wanafunzi bora wa masomo ya sayansi waenda Ireland.

Mwakilishi  kutoka  Ubalozi wa Ireland nchini, Rita Bowen (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi kwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ilongelo  ya Singida, Jafari Ndagula mmoja wa washindi wawili wa jumla wa  shindano la Wanasansi Chipukizi Tanzania 2013 (YST) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Jafari na mwenzake Fidel Samwel (hayupo pichani) wataiwakilisha Tanzania katika sherehe za  Tuzo  za kimataifa za wanasayansi chipukizi duniani mjini Dublin Ireland. Tuzo za YST  zinadhaminiwa na Ubalozi wa Ireland kwa kushirikiana na Mfuko wa Karimjee Jivanjee Foundation (KJF). Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha na Mwenyekiti wa Mfuko wa KJF, Hatim Karimjee.

SHIRIKA la Irish Aid kwa kushirikiana na Taasisi ya Karimjee Jivanjee “KJF” kwa kufadhili wanafunzi wanne bora toka shule ya sekondari ya Ilongero ya Singida na Fidel Castro ya Pemba kwenda Dublin, Ireland baada ya kuibuka washindi wa jumla katika mashindano ya wanasayansi chipukizi (Young Scientists Tanzania) YST mwaka 2013.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa udhamini na kuwaaga rasmi wanafunzi wao jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Taasisi ya karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee amesema kwamba wanafunzi wawili  kutoka shule ya sekondari ya Ilongelo, Jafari Ndagula na Fidel Samwel walishinda tuzo za jumla katika mashindano ya YST 2013 kwa kufanya utafiti wa mradi wa kilimo cha umwagiliaji kwa njia ya kutumia matone (Recycled Material)

“washindi walipokea zawadi ya fedha taslimu, medali, laptops na sasa ziara ya kwenda Dublin Ireland kuwawakilisha wanafunzi wa kitanzania katika sherehe za kimataifa za wanasayansi chipukizi duniani,” amesema karimjee

“Washindi pia walipata udhamini kutoka Karimjee Jivanjee Foundation kwa ajili ya masomo yao ya chuo kikuu kwa siku zijazo kama sehemu ya jitihada za msingi za kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi ya Tanzania,” alilisitiza.

 Amesema kuwa YST pia iliwapa tuzo wanafunzi wawili , Muslih Othman Khamis na Amne Said Sauti kutoka shule ya Sekondari ya Fidel Castro kutoka Pemba kwa ajili ya utafiti wao wa kisayansi juu ya (ethanol) kwa kutumia miwa.

“matokeo ya utafiti wao yatasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira kwa watu badala ya kutumia kuni au mkaa au kutumia pesa nyingi kununua mafuta ya taa, wanaweza kutumia ethanol iliyotengezwa kutokana na miwa ambayo inapatikana kwa wingi huko Pemba,” amesema

” KJF wamekuwa wakisaidia YST tangu 2012 na kuwa mdhamini mkuu na mwaka 2013 KJF waliongeza msaada wake kwa YST kwa kutoa udhamini kwa washindi wa ujumla ikiwa ni pamoja na masomo ya juu kwa ajili ya wale wanaohitaji,” aliongeza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ofisi ya Kamishina wa Elimu, Hadija Mcheka amesema kuwa serikali inaunga mkono kwa ukamilifu mpango ulioanzishwa na YST kwa sababu itaweza kukuza na kuhamasisha wanafunzi kujiingiza katika masomo ya sayansi.

 ”Programu  Hii itakuwa inakuza na kuhamasisha ubunifu miongoni mwa wanafunzi katika nchi wakati jukwaa hili pia litasafisha njia kwa ajili ya wanafunzi kuja pamoja na na kubadilishana uzoefu, ” alieleza.

YST Mkurugenzi Dk Gosbert Kamugisha amesema kuwa waliamua kuja na mpango huo kutokana na ukweli kwamba matokeo ya kidato cha nne na sita kwenye masomo ya sayansi yalikuwa yakishuka siku hadi siku.

Amesema, ” YST ” iliwakutanisha wanafunzi 120 na 60 kutoka shule za sekondari katika mikoa ipatayo 18 na mashindano hayo yalifanyika
mwezi wa Septemba mwaka jana.

Dkt Kamugisha amesema mpango huo ni jukwaa murua kwa wanafunzi  wa shule za sekondari kuja pamoja kuchunguza nadharia, kugundua teknolojia mpya na kuendeleza elimu kisayansi kwa njia ya utafiti na uvumbuzi.

“Kwa vitendo mpango wa kulea wanasayansi vijana kutoka hatua mapema na kuelimisha umma kwa ujumla juu ya umuhimu wa sayansi katika maisha ya kila siku na maendeleo ya kiuchumi, ” amesema.

No comments:

Post a Comment