Mkurugenzi wa chuo kikuu huria tawi la mkoa wa Singida, Bw. Mbaraka Msangi, akitoa taarifa yake kwenye sherehe za kuwapongeza wahitimu 52 wa chuo hicho zilizofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa Katoliki mjini Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Paresko Vicent Kone, akizungumza kwenye kilele cha sherehe ya kuwapongeza wahitimu wa chuo kikuu huria cha mkoa wa Singida,zilizofanyika mwishoni mwa juma mjini Singida.Wa kwanza kulia ni mkurugenzi wa chuo hicho,Mbaraka Msangi.
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone (kushoto) akimkabidhi Mwalimu Allan Jumbe cheti cha kuhitimu chuo kikuu huria mjini Singida.Kwa mwaka huu,jumla ya wanafunzi 52 wamefanikiwa kuhitimu katika chuo hicho.
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa chuo kikuu huria tawi la Singida. Sherehe ya kupongeza wahitimu hao,ilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa katoliki mjini Singida.MKUU wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicenti Kone amewakumbusha wakazi wa mkoa huo umuhimu wa kujiunga na chuo kikuu huria tawi la mkoani humo ili kujiendeleza kielimu.
Amesema kujiendeleza kielimu kutasaidia mhusika kujijengea mazingira mazuri ya kumudu maisha yake kwenye dunia hii iliyojaa ushindani wa kila aina.
Dk.Kone ametoa wito huo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye hafla fupi ya kuwapongeza wahitimu wa chuo kikuu huria kituo cha mkoa wa Singida wa mwaka jana.
Amesema changamoto zinazojitokeza hivi sasa Tanzania,Afrika mashariki na duniani kwa ujumla pamoja na maendeleo ya kisayansi na teknolojia zinatulazimisha sisi wote kuwa na elimu ya kutosha ili kuzikabili.
“Watanzania tusipokuwa na elimu ya kutosha tutaachwa mbali sana na wenzetu wa nchi zinazotuzunguka na wa dunia kwa ujumla.Tusisubiri jambo hili likatokea ili hata jumuiya ya Afrika mashariki itakapokamilika tusije tukakuta nafasi nyingi za kazi zinachukuliwa na wenzetu badala ya vijana wetu,alifafanua Mkuu huyo wa mkoa.
Dk.Kone amesema kutokana na ukweli huo wazazi na walezi wanalo jukumu la kuwashauri na kuwahimiza vijana wao kujiendeleza kwa nguvu zote ili kupata elimu inayokidhi mahitaji ya sasa na yajayo.
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa mkoa amewataka kupuuza dhana potofu kuwa elimu inayotolewa na chuo kikuu huria siyo ya kiwango cha juu bali ni ya kihuria huria tu.
“Dhana hii potofu inayoenezwa kwa lengo la kuwakatisha tamaa Watanzania walio wengi wasipate
elimu ya juu ili kuwe na wachache tu waliosoma na walio wengi wabakie bila elimu”,amesema.
Awali Mkurugenzi wa kituo cha Chuo Kikuu Huria Mkoa wa Singida,Mbaraka Msangi amesema wahitimu wa mwaka huu ni 56 wakilinganishwa na 46 wa mwaka jana.Toka kituo hicho kianzishwe mwaka 2000,hadi sasa wahitimu wameishafikia 263.
No comments:
Post a Comment