Wednesday, January 22, 2014

Vyama vya soka mikoani vyatakiwa kukuza vipaji vya vijana.

 Makamu rais TTF Taifa,Wallace Karia (wa tatu kulia) akiwa kwenye meza kuu pamoja na viongozi wanzake muda mfupi kabla hajafungua mafunzo yaliyohudhuriwa na viongozi wa TFF mikoa mbalimbali hapa nchini jana (18/1/2014).Kulia ni katibu TFF mkoa wa Singida,Hussein Mwamba,anayefuatia ni mwenyekiti TFF mkoa wa Singida, Baltazar Kimario.Wa tatu kushoto  ni Nasibu Ramadhani mjumbe wa kamati ya utendaji TFF taifa na wa pili kushoto ni Wilfred Kidau,mjumbe wa kamati ya utendaji TFF taifa.Mada zilizotolewa kwenye mafunzo hayo ni utawala,ukaguzi wa taarifa za fedha na maendeleo ya timu ya soka ya vijana.
Makamu rais wa TFF taifa,Wallece Karia, akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili yanayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa Katala hotel beach iliyopo mjini Singida.

VYAMA vya soka mikoani vimetakiwa kuweka mikakati madhubuti itakayosaidia kuwajengea vijana mazingira mazuri ya kuibua vipaji vyao ili waweze kuendelezwa kwa lengo la kupata timu bora ya Taifa stars.

Hayo yanasemwa hivi karibuni na Makamu Rais wa TFF taifa,Wallace Kiria,wakati akifungua mafunzo ya siku mbili yaliyohudhuriwa na viongozi wa TFF kutoka mikoani yanayofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Katala Hotel Beach mjini hapa.Mafunzo hayo yalihusu utawala,ukaguzi wa taarifa za fedha na maendeleo ya soka la vijana.

Kiria amesema vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini wenye vipaji vya soka wakiendelezwa,watasaidia kuunda timu bora ya Taifa stars itakayokuwa na uwezo wa kutoa  ushindani wa kweli na sio ya kusindikiza.

 “Watanzania wamechoka au wamechoshwa na mwenendo wa Taifa stars wa kila inaposhiriki mashindano yoyote inatolewa mapema uongozi huu mpya wa TFF malengo yake ni kuona Taifa stars inayotoa ushindani wa hali ya juu na ikiwezekana ianze kuleta makombe mbalimbali nchini mapema”,amesema.

Aidha,Karia amesema kuwa maandalizi hayo ya kuendeleza vijana hasa chini ya miaka 17,ni kuandaa mapema timu ya vijana ambayo itashiriki mashindano ya bara hili la Afrika ambayo, Tanzania itaomba mashindano ya mwaka
2019,yafanyike Tanzania.

Kuhusu mafunzo hayo,amesema kuwa ni mwendelezo wa mafunzo yaliyoanza kutolewa Zanzibar ambayo pamoja na mambo mengine,kuwaongezea uwezo viongozi ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

“TFF ya sasa inataka kufanya kazi moja kwa  moja na viongozi, wadau mbalimbali wa soka ili kufikia malengo tarajiwa kwa ufanisi mkubwa.Tunapaswa tuonyeshe tunaongoza mchezo wa mpira mpya,soka lenye malengo lenye kutoa burudani na kuleta nchini makombe mbalimbali”,amesema.

Wakati huo huo,Makamu huyo wa rais,ameitaka mikoa itakayoandaa mikutano ya TFF taifa,iweke utaratibu wa kuandaa wajumbe kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii.

Kwa mujibu wa Karia,TFF taifa,inatarajia kufanya mkutano wake mkuu mkoani Singida Aprili mwaka huu.

No comments:

Post a Comment