Monday, January 27, 2014

Mvua ya mawe yaharibu ekari 800 za mazao mbalimbali Ikungi.


Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Hassan Tati akikagua mashamba ya mazao mbali mbali yaliyoharibiwa na mvua kubwa ya mawe na upepo mkali iliyonyesha juzi katika kijiji cha Siuyu.Jumla la ekari zai ya 800 zilimeharibiwa na mvua hiyo.

ZAIDI ya ekari 800 za mazao mbalimbali yaliyolimwa katika vitongoji vinne vya kijiji cha Siuyu tarafa ya Mungaa wilaya ya Ikungi,zimeharibiwa vibaya na mvua kubwa ya mawe na iliyoambatana na upepo mkali.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Afisa Mtendaji wa kijiji cha Unyankhanya wilaya ya Ikungi,Adriano Herman wakati akitoa taarifa ya uharibifu mkubwa wa mazao kwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ikungi,Hassan Tati.

Amesema mvua hiyo iliyonyesha juzi usiku kuanzia saa 1.30 jioni hadi saa 2.48 usiku pia ilisababisha nyumba tatu kuanguka chini.

“Mvua hii ilionyesha mapema kwamba sio ya kheri kutokana na upepo wake kuwa mkali mno.Pia ilidondosha mabonge makubwa ya barafu ambayo yalichukua siku nzima kuyeyuka.Kwa ujumla imeharibu ekari 843,213 ya mazao mbalimbali”,amesema.

Herman alitaja mazao yaliyoharibiwa na ekari zake kwenye mabano kuwa ni viazi vitamu (12),mtama (262),uwele (93),alizeti (37.5),maharage (92.5),mahindi (137),ulezi (201.5) na karanga (7.5).

Pamoja na kuwapa pole wakazi hao,Mwenyekiti Tati aliwahakikishia kuwa halmashauri ya wilaya ya Ikungi,inafanya maandalizi ya kuwasaidia mbegu bora za mazao yanayokomaa kwa muda mfupi.

Aidha, Tati amewataka kuendelea kufuata masharti na ushauri wa watalaam wa kilimo ili waweze kupata mavuno ya kukidhi mahitaji.


“Nitumie fursa hii
kuwakumbusha wakulima wote wa wilaya ya Ikungi,kuhakikisha wanalima mazao ya chakula na biashara yaliyopewa kipaumbele na mkoa wetu”,amesema mwenyekiti huyo wa CCM.

No comments:

Post a Comment