Mstahiki meya wa manispaa ya
Singida Sheikh Salum Mahami (katikati) akizungumza kwenye kikao cha
Baraza la Madiwani Mkoani Singida.
Pantaleo Sorongai, Diwani wa
Mitunduruni akimlalamikia mhandisi wa manispaa Singida Robart Massoro
kutokana na utendaji mbovu wa kazi zake
Baraza
la madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Singida limetoa tamko rasmi
kwamba halimhitaji tena mhandisi wa ujenzi Robert Masoro, kwa madai
kwamba utendaji wake haukidhi matarajio ya wakazi wa manispaa hiyo.
Tamko
hilo limetolewa na mstahiki meya wa manispaa ya Singida Sheikh Salum
Mahami, mbele ya kikao cha baraza la madwaini, kilichofanyikia kwenye
ukumbi wa mikutnao wa FDC mjini Singida.
Mapema
wakati baraza hilo linaendelea, yalitokea malalamiko mengi kutoka kwa
madiwani kwamba kazi nyingi zinazosimamiwa na mhandisi Masoro, zimekuwa
chini ya kiwango, kitendo walichodai kuwa manispaa hiyo inaingia hasara
kubwa.
Imedaiwa
zaidi kwamba kazi anazozisimamia mhandisi huyo, zikiwemo za ujenzi wa
barabara, zimekuwa hazifanani na thamani ya fedha zilizotumika.
Baada
ya kumaliza kikao hicho cha kamati ambacho kilichukua zaidi ya saa moja
na nusu, ndipo Meya sheikh Mahami alipotoa tamko hilo.
Sheikh
Mahami ambaye pia ni Sheikh wa mkoa wa Singida, amesema mhandisi Masoro
pamoja na mambo mengine, amekuwa na manyanyaso ya wazi wazi dhidi ya
makandarasi.
Mhandisi Masoro amekuwa akikumbwa na misuko suko mingi katika utendaji wake wa kazi.
Hivi
karibuni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu, Kapteni Honest
alikosoa miradi yote iliyiosimamiwa na mhandisi Masoro na kuahidi
kuchukua jina lake na kulipeleka katika ngazi za juu kwa maamuzi zaidi.
No comments:
Post a Comment