Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida Linuys Sinzumwa akitoa taarifa kwa waandishi
wa habari (hawapo kwenye picha) ya ajali iliyoua vijana wawili ndugu.
Vijana
wawili wa familia moja wakazi wa kijiji cha Mwankoko manispaa ya
Singida wamegongwa na gari aina ya Land Rover na kufariki dunia papo
hapo.
Vijana hao ni Seleman Juma (42) na Mohammede Juma (33).
Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa amesema vijana hao wamegongwa
Agosti 29 mwaka huu katika barabara ya Singida mjini – Kindaa eneo la
kijiji cha Mwankoko.
Amesema
siku ya tukio, vijana hao wakiwa na baskeli zao wakitokea kitongoji cha
Isomia kata ya Mwankoko wakielekea Singida mjini, waligongwa na Land
Rover T.501 ASG ambayo iliwafuata hadi nje ya barabara.
Akifafanua,
Sinzumwa amesema Land Rover hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na dereva ambaye
hadi sasa jina lake halijafahamika, liliacha barabara na kuwafuata
vijana hao ambao walikuwa nje ya barabara na kuwagonga na kusababisha
vifo vyao papo hapo.
Sinzumwa amesema tayari wameanzisha msako mkali wa kumsaka dereva huyo akamatwe na kisha kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Katika
hatua nyingine, Kamanda huyo amesema kuwa jumla ya waumini wa kiislamu
wanne, wanashikiliwa kwa tuhuma ya kugoma kushiriki zoezi la sensa.
Amewataja
waumini hao kuwa ni Jidawi Ramadhani (31), Hussein Juma (23), Saidi
Maulid (19) na Hamisi Shaban (18) wote ni wakazi wa Singida mjini.
Amesema watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya kugoma kutoa taarifa zao kwa makarani wa sensa.
No comments:
Post a Comment