Mhudumu
wa chuo cha VETA mjini Singida Maria Chilinde akiwa wodini katika
hospitali ya mkoa akipatiwa matibabu ya majeraha baada ya kukatwa katwa
visu na mchumba wake.
Kijana
mmoja mkazi wa mkoa wa Dodoma aliyetambulika kwa jina moja la Oscar
anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 24, amejiuwa kwa kutumia pazia la
dirisha.
Oscar
amejiuwa oktoba 13 mwaka huu usiku wa kuamkia leo muda mfupi baada ya
kumkatakata vibaya mchumba wake Maria Chilinde (25).Maria ni mhudumu
wa chuo cha VETA Mjini Singida, na amepata dhahama hiyo kwenye nyumba
anayoishi ya VETA.
Maria
ambaye amepoteza damu nyingi zilizosababishwa na majeraha ,
amelazwa wodi namba mbili, katika Hospitali ya Mkoa iliopo mjini
Singida.
Kwa
mujibu wa muuguzi wa wodi hiyo ambaye ameomba jina lake lisitajwe
kwa madai kwamba sio msemaji wa hospitali hiyo, alisema hali ya Maria
inaridhisha na akadai akimaliza chupa ya damu aliyotundikiwa, anaweza
kuanza kuongea.
Akifafanua zaidi,alisema Maria ana majeraha makubwa Kichwani,mkononi, na sehemu za mbavu.
Habari
za uhakika kutoka eneo la tukio zinadai kuwa Oscar (marehemu), ana
kawaida ya kumtembelea Maria mara kwa mara. Wakati mwingine alikuwa
akimaliza mwezi akiwa na mchumba wake.
Hata
hivyo inadaiwa kuwa kuna kipindi wazazi wa Maria walikuwa wanadai
walipwe mahari ya shilingi milioni mbili na Oscar,ili aweze kuruhusiwa
kumwoa Maria.
Habari
zaidi zinadai kuwa baada ya kijana Oscar alishindwa kutoa mahari
hiyo ya shilingi milioni mbili kitendo kilichopelekea wazazi waanze
kukataa binti yao kuolewa na Ocsar.
Habari hizo zinadai kuwa kitendo hicho kilichasababisha kijana huyo atake kumuuwa mchumba wake na kisha yeye naye ajiuwe.
Oscar baada ya kumcharanga mchumba wake Maria kwa kisu na kusababisha azirai, alihisi Maria ameishafariki dunia.
Baada
ya Oscar kuhisi Maria amefariki dunia alichukua kipande cha pazia
akapanda juu ya stuli kisha kufunga pazia kwenye kenchi. Zoezi hilo
lilipomalizika la kujitundika alisukuma stuli pembeni kuanza
kuning’inia na kupelekea kupoteza maisha yake.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,Linus Sinzumwa amekiri kutokea kwa tukio hilo na amedai upelelezi zaidi unaendelea.
No comments:
Post a Comment