Kaimu meneja wa mamlaka ya
chakula na dawa kanda ya kati(TFDA), Aberl Deule akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya zoezi la kukagua bidhaa
katika maduka ya wilaya ya Manyoni.
Moto ukiwa umewaka kuteketeza bidhaa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tano ambazo ni sumu na zile ambazo muda wake wa kutumika umekwisha.Bidhaa hizo zilikamatwa na TFDA katika baadhi ya maduka ya wilaya ya Manyoni.
Bidhaa ambazo zina sumu na zilizokwisha muda wake zilizokamatwa na TFDA kabla hazijateketezwa kwa moto.
Kaimu meneja wa TFDA kanda ya kati, Aberl Deule (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa muuza duka wa Manyoni mjini.
Moto ukiwa umewaka kuteketeza bidhaa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tano ambazo ni sumu na zile ambazo muda wake wa kutumika umekwisha.Bidhaa hizo zilikamatwa na TFDA katika baadhi ya maduka ya wilaya ya Manyoni.
Bidhaa ambazo zina sumu na zilizokwisha muda wake zilizokamatwa na TFDA kabla hazijateketezwa kwa moto.
Kaimu meneja wa TFDA kanda ya kati, Aberl Deule (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa muuza duka wa Manyoni mjini.
Mamlaka
ya Chakula na Dawa Kanda ya Kati (TFDA) imeteketeza bidhaa mbali mbali
zenye thamnai ya zaidi ya shilingi milioni tano zikiwemo zile ambazo
muda wake wa kutumika umeisha.
Bidhaa
hizo ni pamoja na soda, juice, biskuti (muda wake wa kutumika
uliishapita) na maziwa ya unga ya watoto wadogo aina ya Lactogen (18 na
2) ambayo ni bandia.
Bidhaa
zingie zilizoteketezwa ni tani moja ya vipodozi hatari kwa matumizi ya
binadamu yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tatu.
Vipodozi hivyo vyenye kemikali za hydroquinone na zebaki, hutumiwa kubadilisha rangi ya ngozi (kujichubua).
Akizungumza
muda mfupi baada ya kuteketeza bidhaa hizo, Kaimu Meneja TFDA Kanda ya
Kati Aberl Deule, amesema msako wa ukaguzi wa kuangalia ubora na usalama
wa chakula, dawa na vipodozi, ulianza Novemba 13 hadi 17 wilayani
Manyoni.
Amesema
msako huo ambao ni endelevu, ulifanyika katika maeneo 52 ya Manyoni
mjini na Itigi, ambayo ni pamoja na viwanda vya kutengeneza vyakula,
kuuzia vyakula, maduka ya vipodozi, maduka ya dawa za binadamu na yale
ya dawa za mifugo.
Katika
hatua nyingine, Kaimu Meneja huyo amewataka wananchi kuhakikisha
wanatumia bidhaa ambao hazijaisha muda wake na zile ambazo hazina sumu.
Kwa
upande wa wafanyabiashara, Deule amewataka muda wote wahakikishe
wanampatia mteja bidhaa zenye ubora, zisizokuwa na sumu na zile ambazo
muda wake wa kutumika, haujaisha.
Amesema
“Wafanyabiashara mnaojishughulisha na biashara za chakula, dawa,
vipodozi na vifaa tiba, hakikisheni majengo yenu yanasajiliwa na TFDA.
Hakikisheni pia bidhaa, mnazozalisha au kuuza ni salama kwa afya ya
binadamu na bora”.
Deule
amewataka wajenge utamaduni wa kukagua bidhaa zao ili kubaini kama
kuna bidhaa zilizopitwa muda wa matumizi na wajiepushe kuuza vipodozi
vyenye viambato vya sumu.
Imedaiwa
kuwa mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina moja la Anord wa Manyoni
mjini, amelazwa katika hospitali ya wilaya, muda mfupi baada ya
shehena ya biadhaa zisizokuwa salama kwa matumizi ya binadamu, kuamatwa
dukani kwake.
No comments:
Post a Comment