Mhadhiri wa chuo kikuu
Dar-es-salaam, Dk.Kitila Mkumbo (kushoto) akitetea jambo na wakili wake
Raymond Kimu muda mfupi kabla hajasomewa shitaka lake la kutoa lugha ya
matusi kwa mbunge wa jimbo la Iramba magharibi Mwigullu Nchemba.
Kesi
inayowakabili vigogo wawili wa CHADEMA taifa, imeaahirishwa hadi
Desemba 17 mwaka huu kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na
mwanasheria wa serikali kuugua.
Imeelezwa
mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Ruth Massamu, kuwa
mwanasheria huyo wa serikali Maria Mdulugu anayesimamia kesi hiyo ni
mgonjwa.
Vigogo
hao ambao wanatuhumiwa kumtolea lugha ya matusi mbunge wa jimbo la
Iramba magharibi Mh. Mwigulu NChemba ni Afisa Sera na Utafiti makao
makuu Waitara Mwikwabe (37) na Mhadhiri wa chuo kikuu Dar-es-salaam na
mshauri wa CHADEMA Dkt. Kitila Mkumbo.
Kwa
mujiubu wa mwanasheria wa serikali Seif Ahmed, washitakiwa bila halali,
walimtusi mbunge Mwigullu kuwa ni malaya, mzinzi na mpumbavu huku
akijuwa wazi kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria.
Seif
amesema kuwa washitakiwa hao bila halali, walitenda kosa hilo kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nguvumali kwa lengo la
viongozi wa CHADEMA kuzungumza na wananchi.
No comments:
Post a Comment