Kata
ya Ipembe jimbo la Singida mjini inakabiliwa na uhaba mkubwa wa nyumba
za kuishi walimu zipatazo 72 katika shule zake tatu ikiwemo moja ya
sekondari.
Akitoa
taarifa yake ya utekelezaji mbele ya kikao cha baraza la madiwani wa
manispaa ya Singida, diwani wa kata hiyo Twalib Kihara amesema shule ya
msingi Ipembe inakabiliwa na upungufu wa nyumba za kuishi walimu 23,
wakati shule ya msingi Sumaye, pia ina upungufu wa nyumba 20.
Kihara
amesema shule pekee ya sekondari ya kata hiyo, inahitaji nyumba za
kuishi walimu 30, kwa sasa ina nyumba moja tu, na hivyo inakabiliwa na
upungufu wa nyumba 29.
Katika
hatua nyingine, Kihara ametaja baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa
ni pamoja na upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi katika shule ya
sekondari Ipembe.
Diwani
huyo mkongwe,alitaja changamoto zingine kuwa ni uhaba wa vitendea kazi
na mwitikio mdogo wa jamii katika uchangiaji wa maendeleo.
Kwa
mujibu wa diwani Kihara Kata ya Ipembe ni miongoni mwa kata 16 za
manispaa na ina wakazi wapatao 2,833 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002.
Ndugu nashukuru kwa habari zako nzuri tunazopata katika blog yako hii nzuri, lakini ninachoomba kwako picha za SGD mjini ili hata mtu akipitia blog hii aione SGD yetu na sisi wa ughaibuni tuione tufurahi kidogo.
ReplyDelete