Mshitakiwa wa kwanza Bw. Mwita
Waitara Mwikwabe (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye bechi wakisubiri
kuitwa mbele ya hakimu Ruth Massamu.
Vigogo wa CHADEMA washitakiwa
Mwita Waitara Mwikwabe (wa pili kulia) na mshitakiwa wa pili,Dk.Kitila
Mkumbo (wa kwanza kushoto mwenye miwani), wakitoka nje ya mahamaka ya
hakimu mkazi Singida mjini,baada ya kesi yao kuahirishwa hadi Oktoba 8
mwaka huu.
Kesi
inayowakabili vogogo wa CHADEMA ya kumtolea lugha ya matusi mbuge wa
jimbo la Iramba Magharibi, Mwigullu Lameck Nchema inatarajiwa kuanza
kuuguruma leo asubuhi (5/11/2012) kwenye mahakama ya hakimu mkazi mjini
Singida.
Upelelezi wa kesi hiyo,uliishakamilika na uchambuzi wa awali ulifanyika Septemba tatu mwaka huu.
Vigogo
hao wanaotuhumiwa kutenda kosa hilo julai 14 mwaka huu saa kumi
jioni,ni afisa sera CHADEMA makoa makuu,Mwita Waitara Mwikwabe (37) na
mshauri wa CHADEMA na mhadhiri wa chuo kikuu Dar-es-salaam,Dk.Kitila
Mkumbo (41).
Kesi hiyo inayovutia hisia na watu wengi,inasikilizwa na hakimu,Ruth Massamu,wa mahakama ya mkoa wa Singida.
Kwa
mujiubu wa mwanasheria wa serikali,Seif Ahmed,washitakiwa bila
halali,walimtusi mbunge Mwigullu kuwa ni malaya, mzinzi na mpumbavu huku
akijuwa wazi kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria.
Seif
alisema kuwa washitakiwa hao bila halali alitenda kosa hilo kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nguvumali kwa lengo la
viongozi wa CHADEMA kuzungumza na wananchi.
No comments:
Post a Comment