Tuesday, November 13, 2012

MKAZI WA SINGIDA AKUTWA AMEJINYONGA KWA KUTUMIA WAYA.

 Kijana wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 28 na 33 mfanyabiashara za machinga mjini Singida,Bakari Kavite,mwili wake umeokotwa saa moja na nusu  akiwa amejinyonga kwenye nyumba ya sinema ya Furaha jirani na hotel yenye hadhi ya kitalii ya Stanely motel.Amejinyonga hadi kufa kwa kutumia waya.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida,Linus Sinzumwa,ameahidi kutoa taarifa baadaye kuhusiana na tukio hilo.
 Askari na Wakazi wa Singida wakibeba mwili wa Marehemu kuupeleka Hospital kwa ajili ya uchunguzi.

                               Wananchi wakiwa wamekusanyika eneo la tukio.

No comments:

Post a Comment