WATU watatu wa familia
moja wamefariki duniani mkoani Singida baada ya kuangukiwa na nyumba.
Kamanda wa polisi mkoa
wa Singida kamishina msaidizi Linus Sinzumwa amesema tukio hilo limetokea
jana majira ya saa 10 alfajiri wakati wanafamialia hao wakiwa
wamelala.
Amewataja waliokufa kuwa
ni baba wa familia hiyo Ramadhani Amrani (25) mkewe
Mariam Kondo (23) na mtoto wao Amrani Ramadhani mwenye
umri wa miezi saba wote wakazi wa eneo la Tambuka-Reli katika halshauri
ya wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
Kamanda Sinzumwa amesema
siku ya tukio wanafamilia hao walikuwa wamelala kwenye nyumba yao
waliyojenga kwa tofali mbili na kuezeeka kwa miti na udogo mwezi mmoja
uliopita.
Hata hivyo amesema
kutokana na kile kinachosadikiwa kuwa kuzidishwa udogo juu, miti
iliyotumika kujengea nyumba hiyo ilivunjika, hali iliyosababisha udogo na kuta
kuporomoka.
Kamanda Sinzumwa
amesema hali hiyo ilisababisha wanafamilia hao watatu kukandamizwa
na kupondwa na miti, tofali na udogo hadi wakapoteza maisha yao
papo hapo.
No comments:
Post a Comment