Mkazi wa Mwasauya mkoani Singida amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kubainika kutenda kosa wizi wa mifugo.
Akisoma hukumu hiyo hakimu wa mahakama ya mwanzo utemini Joyce Shilla amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Msunga Sima kuwa alitenda kosa hilo september 28 mwaka huu.
Hakimu Shilla amesema mshitakiwa akiwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Rajabu Sidadi waliiba mbuzi wawili na kisha kumchinja mmoja kabla ya
mtuhumiwa rajabu kutoroka na kukimbilia kusiko julikana
Mtuhumiwa amehukumiwa kifungo cha miaka mitano na faini ya shilingi laki moja na elfu ishirini
No comments:
Post a Comment