Na SingidaYetu.Blogspot.com
Wajumbe wa jumuiya ya tawala za mikoa Tanzania ALAT mkoa wa Singida wametakiwa kuonyesha uwezo wa kukusanya mapato yanayotokana na Ada za lesen kwa ukamirifu ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa
Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone wakati wa ufunguzi wa Kikao cha ALAT mkoa kilichofanyika kwenye ukumbi wa parokia ya kanisa katoliki mjini Singida
Dr. Kone amesema ada za lesen zikikusanywa kwa ukamilifu serikal itaongezea halmashauri za mkoa wa Singida wigo mpana wa vyanzo katika halmashauri zote
Amesema kwa kutumia fursa hiyo ya makusanyo kutasaidia kuwa na matokeo chanya kwa kuibua,kukusanya kusimamia na kufuatilia mapato ya halmashauri.
No comments:
Post a Comment