Thursday, October 3, 2013

Washirikisheni watumishi wa umma katika ngazi za maamuzi – Kombani

 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais na Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mh. Celina Kombani (wa pili kulia) akishiriki kuimba wimbo wa umoja wa wafanyakazi muda mfupi kabla ya kufungua kikao cha 16 cha baraza la wafanyakazi wa chuo cha watumishi wa umma Tanzania.Wa kwanza kulia ni Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida, mwalimu Queen Mlozi.
 Baadhi ya watumishi wa chuo cha Utumishi wa Umma wakishiriki kuimba wimbo wa umoja wa wafanyakazi muda mfupi babla ya kikao cha 16 cha baraza la wafanyakazi wa chuo cha watumishi wa umma Tanzania kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Katala Beach mjini Singida.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mh. Celina Kombani, akizungumza katika ufunguzi wa kikao cha 16 cha baraza la wafanyakazi wa chuo cha utumishi wa umma Tanzania kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Katala Beach Singida mjini.Kulia ni kaimu mkuu wa mkoa wa Singida,mwalimu Queen Mlozi na kushoto ni mkuu wa chuo cha utumishi wa umma Tanzania na mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi, Saidi Nassoro.
 Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa chuo cha utumishi wa umma, wakisikiliza kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa kwenye kikao cha 16 cha baraza la wafanyaka kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Katala Beach mjini Singida.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mh. Celina Kombani (wa nne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kikao cha 16 cha baraza la wafanyakazi wa chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania. Wa watatu kulia ni kaimu mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya ya Singida, mwalimu Queen Mlozi.Wa kwanza kulia ni afisa sekratieti  serikali za mitaa Willbord Marandu na anayefuata ni mwenyekiti wa TUGHE taifa Dk.Diwani Mrutu.Wa tatu kushoto ni mkuu wa chuo cha utumishi wa umma Tanzania na mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi,Saidi Nassoro.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Menejimenti ya Utumishi wa Umma,Celina Kombani,amekiangiza chuo cha utumishi wa umma na taasisi zake zihakikishe ushirikishwaji wa watumishi katika kufanya maamuzi muhimu mahala pa kazi unapewa nafasi.

Amesema ushirikishwaji huo utaongeza ufuatiliaji wa utekelezaji wa maamuzi yanayofanywa, ili kuongeza mafanikio na maendeleo ya taasisi husika, ikiwemo chuo cha utumishi wa umma.

Waziri Kombani ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao cha 16 cha baraza la wafanyakazi wa chuo cha watumishi wa umma Tanzania kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Katala beach mjini Singida.

Akifafanua zaidi,waziri Kombani amesema ushirikishwaji huo utaongeza uzalishaji, kuimarika kwa nidhamu, uwajibikaji, kukomaa kwa demokrasia mahali pa kazi na kujenga mahusiano bora kazini.

“Pia ushirikishwaji huu wa watumishi katika kufanya maamuzi muhimu mahali pa kazi,utasaidia kujenga maadili ya watumishi wa umma na kutoa huduma bora kwa
wateja na wadau wa chuo pamoja na kuboresha maslahi ya watumishi”,amesema.

Aidha, Kombani amesema ushirikishwaji wa watumishi katika maamuzi mbalimbali ya kiuongozi, utumike katika kijizatiti na kutatua changamoto za taasisi husika na kuongeza uwajibikaji katika kuhudumia umma wa Watanzania kwa unyenyekevu.

“Napenda kusisitiza kwamba tija na ufanisi, ndiyo viwe vigezo na vipimo vya kwanza vya vikao vya mabaraza, vitapelekea kuangalia maboresho ya maslahi ya watumishi. Kwani uzalishaji duni utasaidia maslahi kwa watumishi”,amesema.

Kombani alitumia fursa hiyo kuwahimiza na kuwaasa waajiri wakitumie chuo cha utumishi wa umma Tanzania kupata mafunzo muhimu kwa waajiriwa wao.

“Mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya yatolewayo na chuo chetu cha utumishi ni muhimu mno ili kuweza kuongeza ufanisi katika taasisi za umma na kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa Watanzania”,alifafanua Waziri Kombani.

No comments:

Post a Comment