Sunday, October 20, 2013

FAMILIA YANUSURIKA KIFO BAADA YA KIMBUNGA KUEZUA NYUMBA MKOANI SINGIDA




Familia moja imenusurika kufa kufuatia kimbunga kuezua nyumba wanamoishi ,katika wilaya ya ikungi mkoani singida. Tukio hilo limetokea jana majira ya saa kumi na nusu jioni, katika kijiji cha choda kata ya mkiwa tarafa ya Ikungi.

Akizungumza na Singidayetu.blogspot.com diawani wa kata ya mkiwa Bw. Mathias Sungita, ametaja walionusurika kuwa ni familia ya  Bw Saimon Joram.

Imelezwa kuwa upepo mkali uliofuatana na kimbunga ulizingira nyumba ya Bw Sungita, na
kuezua paa wakati familia hiyo ikiwa ndani.
Wananchi wametakiwa kutoa msaada kwa familia hiyo ambayo kwa sasa haina sehemu ya kuishi.

No comments:

Post a Comment