Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida Yahaya Nawanda akizungumza na mwandishi wa habari wa Singida Yetu Blog (hayupo kwenye picha) juu ya kuagizwa kwa njacho mpya ya ugonjwa wa kideri.
Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida Yahaya Nawanda akilisha baadhi ya kuku wake wa kienyeji kati ya 966 anaowafuga kibiashara, katika eneo la nyumba anayoishi.
WILAYA ya Iramba mkoani Singida imelazimika kuagiza zaidi ya dozi laki nne za chanjo ya ugonjwa wa kideri moja kwa moja toka kiwandani, kwa ajili ya kusambaza kwa wafugaji wa kuku.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya kubainika kuwa dawa na chanjo nyingi zinazonunuliwa na wananchi kwenye maduka binafsi ya kilimo na mifugo zinakuwa zimechakachuliwa na kusababisha kuku kufa.
Akizungumza kwenye mafunzo ya ufugaji bora wa kuku, Mkuu wa Wilaya hiyo Yahaya Nawanda amesema baada ya kubaini tatizo katika chanjo hizo, wameona vyema kuagiza moja kwa moja toka kiwandani zinakotengenezwa na kuzimbaza kwa wananchi wanaofuga kuku Vijijini.
Bwana Nawanda amesema tayari mpango huo umeanza kutekelezwa na dozi hizo za chanjo zaidi ya laki nne zinatarajiwa kuwa zimewasili katika Wilaya ya Iramba kabla ya
mwisho wa mwezi huu.
Ufugaji wa kuku wa asili ni moja shughuli kuu za kiuchumi kwa wananchi wa mkoa wa Singida ambapo inakadriwa kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana zaidi ya kuu milioni mbili walikuwa wanafugwa.

No comments:
Post a Comment