Friday, October 25, 2013

Halmashauri ya Singida kunufaika na mradi wa barabara unaofadhiliwa na benki ya dunia.


Kampuni ya Kichina ya SIETCO ikijenga kwa kiwango cha lami barabara ya Singida hadi kijiji cha Mwankoko Barabara hiyo ni moja kati ya barabara zinazojengwa kwa kiwango cha lami kwa ufadhili  wa Benki ya Dunia.

Halmashauri ya Manispaa ya Singida itanufaika na mradi wa uimarishaji na uendelezaji wa miundombinu ya barabara yenye urefu wa kilometa 15.32 kwa kiwango cha lami unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB).

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida,Joseph Mchina wakati akitoa taarifa yake ya utekelezaji wa kazi za barabara kwa kipindi cha kuanzia februari hadi agosti mwaka huu.

“Jumla ya shilingi 329 milioni tayari zimekwisha tengwa kwa ajili ya kazi ya upembuzi yakinifu,uandaaji makisio na michoro ya kihandisi ya uimarishaji wa miundo mbinu ya barabara zenye urefu wa kilometa 15.32″,amesema Mchina.

Mkurugenzi huyo alizitaja barabara hizo na urefu wake wa kilometa kwenye mabano kuwa ni barabara ya Karume itakayojengwa njia mbili (0.72),Karume – Ukombozi,barabara ya Singida-Dodoma-Arusha (1.3) na barabara ya Boma-Kinyeto (2.7).

Mchina alitaja barabara zingine kuwa ni Makutano ya barabara ya Karume-Dodoma (1.6),Majengo-Karakana -shule ya viziwi(1.7),Mkutano ya barabara ya Karume-soko la zamani la vitunguu-Mwenge DP (0.5) na makutano ya barabara ya Sepuka-Airport-VETA (1.4).

“Zingine ni makutano ya barabara ya Arusha-Karakana ya ujenzi (0.3),barabara ya Semali-kituo kipya cha mabasi (1.1) na makutano ya barabara ya
Mwanza-FDC-NMC (O.9)”,alisema mkurugenzi Mchina.


Halmashauri ya manispaa ya Singida inao mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa 481.139.Kati ya barabara hizo,barabara za changarawe zina urefu wa kilometa 52.83,za udongo kilometa 416.782 na kilometa 11.52 ni za lami.

No comments:

Post a Comment